Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Akili Mne imevumbua dawa za aina mbili za maambukizi (Antibiotics) mpya zinavyoweza kuwaua vimelea vya kisonono sugu na MRSA, watafiti wamefichua.
Dawa hizo ziliundwa Akili Mnemba kwa chembembe chembe ndogo sana na kuua vimelea hao wa maambukizi sugu katika majaribio ya maabara yaliyohusisha Wanyama.
Michanganyiko miwili bado inahitaji miaka ya uboreshaji na majaribio ya kimatibabu kabla ya kutolewa na madaktari kwa wagonjwa
Lakini timu ya Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT) uvumbuzi huu inasema Akili Mnemba inaweza kuanza “enzi mpya ya dhahabu” katika ugunduzi wa dawa za kuua bakteria.
Dawa hizo huua bakteria, lakini maambukizi sugu sasa yanasababisha vifo vya zaidi ya milioni moja kwa mwaka.
Kutumia dawa za bakteria kupita kiasi kumewasaidia bakteria kubadilika ili kuepuka athari za dawa, na kumekuwa na uhaba wa dawa zinazoua bakteria mpya kwa miongo kadhaa.
Uidhinishaji wa mwisho wa mpango wa “udhibiti wa kijeshi” wa Gaza unakaribia

Wanajeshi wa Israel wakiendesha shughuli zao karibu na vifaru kwenye eneo la mkutano karibu na mpaka na Ukanda wa Gaza, Agosti 13, 2025
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yisrael Katz alikutana Alhamisi na Mkuu wa Majeshi wa IDF Eyal Zamir na baadhi ya maafisa wakuu wa Utumishi ili kukagua “mpango wa jeshi wa kuudhibiti kijeshi” mji wa Gaza.
Ni vyema kutambua kwamba mpango wa mwisho utawasilishwa Jumapili ijayo kwa idhini ya mwisho.
Televisheni ya Channel 12 ilimnukuu Zamir akisema, “Haja ya mshikamano kati ya ngazi ni muhimu ili kuhakikisha uamuzi na nguvu ya serikali.”
Pia alisema, “Uhusiano kati ya ngazi ya kisiasa na kijeshi ni mhimili na msingi wa usalama wa taifa, hasa wakati wa vita.”
Mkutano kati ya Zamir na Katz ni sehemu ya mkutano wao wa kawaida wa kila wiki. Zamir anatarajiwa kuidhinisha mipango ya kuchukua udhibiti wa mji wa Gaza Jumapili ijayo, wakati jeshi baadaye litawasilisha mipango ya kina na ratiba ya operesheni hiyo katika ngazi ya kisiasa, kulingana na Mamlaka ya Utangazaji.
Jeshi la Israel lilisema katika taarifa yake kwamba wakati wa mkutano wa Mkuu wa Majeshi na viongozi wa usalama na kijeshi, “wazo kuu la mpango wa hatua zinazofuata katika Ukanda wa Gaza lilipitishwa, kwa mujibu wa maagizo ya kisiasa.”
Baraza la Mawaziri la Usalama liliidhinisha mpango siku ya Ijumaa wa kudhibiti mji wa Gaza na awamu inayofuata ya vita katika eneo la Palestina.
Muda muhimu Alaska: Trump kukutana na Putin huku Ukraine ikitengwa

Maafisa wa Marekani na Urusi watakutana katika jimbo la Alaska kabla ya mkutano wa Ijumaa unaotarajiwa kati ya Rais Donald Trump na Vladimir Putin.
Wawili hao watakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita, huku Trump akijaribu kutunga ahadi muhimu ya kampeni ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.
Rais wa Marekani, ambaye amejionyesha kama mtu wa kuleta amani duniani, anatumaini kuimarisha uhusiano wake wa kibinafsi na Putin ili kufikia muafaka wa kusitisha mapigano ambapo wengine wameshindwa.
Siku ya Alhamisi alikadiria kuwa kwa “fursa ya 25%” mkutano huo hautafanikiwa.
Kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameondolewa kwenye mazungumzo hayo, na kuonya kuwa maazimio yoyote yatakayotolewa bila kuwepo kwake hayatakuwa na maana yoyote.
Huko Anchorage kuna dalili chache za mkutano wa hali ya juu unaokuja, isipokuwa vyombo vya habari vya kimataifa ambavyo vimefika kwenye eneo hilo.
Mkutano wa Ijumaa kati ya viongozi hao wawili utafanyika katika kambi ya kijeshi ya Marekani iliyo karibu – ikiwa ni taswira ya wasiwasi wa kiusalama na mpango wa kuketi kwa ajili ya mazungumzo hayo umefupishwa, ikipagwa kuwa mkutano huoutadumu kwa saa chache tu.
Mkutano huo unakuja wiki moja baada ya makataa ya Trump yakikaribia kwa Urusi kufikia usitishaji vita au kukabiliwa na vikwazo vipya vikali.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.