Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwaka 1951 mwanasaikolojia maarufu, Solomon Asch alifanya utafiti kuhusiana na uwezo wa watu kusimamia wanachokiamini na kukubali kuwa tofauti na watu wengine.
Katika jaribio hili lililoitwa (Asch Experiment) alichukua watu kadhaa na kuwaweka pamoja kisha kuchora mistari kadhaa kwenye ubao na kuwaambia wasome.
Katika mistari hiyo kuna miwili ambayo ilikuwa lazima ifanane.
Katika watu aliowachukua, wengine wote aliwaeleza kuhusiana na jaribio hilo, isipokuwa mtu mmoja ambaye aliwekwa mwishoni ndiye hakuambiwa kwamba yuko kwenye jaribio.
Wale watu wa kwanza waliokuwa wameambiwa kuhusu jaribio hilo, waliambiwa kila mmoja aseme jibu linalofanana (ambalo halikuwa la kweli) kuhusiana na mstari upi unalingana na upi.
Mistari ilipewa jina na lile jibu la uongo lilikuwa linafanana kwa mbali na ukweli lakini halikuwa sahihi.
Zoezi lilipoanza, mwanzoni wale wa kwanza wote walisema jibu linalofanana na yule wa mwisho alisema la kwake tofauti ambalo lilikuwa sahihi.
Baada ya kuletewa mistari kadhaa mingine ya kulinganisa, yule wa mwisho akaanza kufuatisha wengine majibu wanayoyatoa.
Baada ya jaribio alipoulizwa sababu ya kwanza alisema kuwa, alikuwa anajua kuwa hayuko sahihi ili alikuwa anaogopa kuwa tofauti na wenzake.
Sababu ya pili alisema kuwa, alihisi haiwezekani watu wote wakosee nay eye peke yake ndiye awe sahihi, lazima yeye ndiye atakuwa amekosea.
Kutokana na utafiti huu iligundulika kuwa watu wengi wanaogopa kuwa tofauti na kufanya mambo tofauti kwa sababu:
a. Normative Influence: Watu wanataka “kufit” kwenye Maisha na utaratibu uliozoeleka.
Yaani wengi huogopa kuonekana wa tofauti kwenye maamuzi yao, uchaguzi wa Maisha yao, mwelekeo n.k
b. Informative Influence: Watu hufikiria kuwa kama wengi wanafanya jambo fulani basi wana ufahamu zaidi kuliko wao na haiwezekani kufanikiwa katika kitu tofauti.
Matokeo yake huwa wanalazimika kusikiliza wengine zaidi kuliko kujisikiliza mioyo yao.
Na wewe jikague leo, ni mmoja wa watu ambao wanaogopa kuwa tofauti kwa sababu hizo hapo mbili juu?
Kama una ndoto, Amua kuiamini kuanzia leo na usitishwe na kuendeshwa na mawazo ya wengine ambayo yamesababisha ukaisahau na kuidharau ndoto yako.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.