Unaweza wachwa vitani,kimkakati na Mungu.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna aina fulani ya VITA ambayo Mungu atahakikisha anakuacha unapigana PEKE YAKO, hataruhusu mtu mwingine akusaidie.

Sio kwa sababu anataka ushindwe vita hiyo, ila ni kwa sababu ni vita ya mkakati anataka kukutofautisha na kubadilisha viwango vyako.

Yaaani itakuwa Kama vile hakuna aliye tayari kukusaidia, Hata wale ambao huwa umezoea wanajitolea kuwa na wewe nyakati Kama hizo hautawaona.

Ukiona unapitia kwenye vita Hii, usianze kulalamikia watu au kumlaumu Mungu kuwa amekuacha. Jua kwamba uko kwenye vita ya mkakati.

Mungu huwa Hana upendeleo, ili akupeleke mahali/kiwango ambacho wengine hawajafika lazima atengeneze mazingira ambayo yataonyesha kuwa hajakupendelea (Rudia Kusoma Tena Hii).

Na njia rahisi ya wewe kutoonekana umependelewa ni pale ambapo unapita ambapo wengine hawajapita na hauachi kumtegemea yeye.

Nakuombea, Hata Kama unaona Nguvu zimekuishia, usiishie njiani na usikate tamaa. Siku Yako Imekaribia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment