Jinsi ya upishi.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

“umejifunza lini kupika?” aliuliza mama Mona kwa mshangao, “bibi yake Jack amenifundisha” jibu la Monalisa, alikumshtua mama Mona, kama lilivyo mshtua Monalisa mwenyewe, ambae akutegemea kutamka wazi wazi jina la kijana huyu ambae amemfundisha kwa nini baba na mama wanalala chumba kimoja. . . . . ENDELEA…….

“hoooo!, ulijifunza kupika nini na nini?” anauliza mama Mona, ambae alihakikisha anaonja kilicho pikwa na mwanae, “ubwabwa ugari na mboga” alisema Monalisa, ambae alicho kipika, kilifurahiwa na mama yake, ambae akujuwa sababu ya radha ya embe, kutawara kwenye ile supu.

Monalisa ambae akuishia kwenye kupenda supu ya embe bichi, ila pia alipenda sana kutumia vitu vyenye ugwadu, asa limao, mbilimbi na machungwa machachu, ambayo alikuwa anaagiza kila dada yao wakazi, yani Khadija alipoenda sokoni, wakati mwingine ali.

Siku chache mbele, bwana Edson, ambae ni mmoja kati ya wajumbe ya kamati ya ushauri kwa mfalme, yani baba yake Monalisa, ambae pia, mapenzi yake kwa binti yake ni makubwa sana, akiwa amefika dar, kwa mapumziko ya week mbili, akitokea Mbogoland

Week moja, mama Monalisa, anaitaji kumwonyesha mume wake, jambo ambalo alimsimulia siku moja usiku, jambo ambalo wote wawili walilifurahia kwa kuona binti yao amekuwa mdada wenye uwezo wakufanya majukumu muhimu ya kike.

Ndipo mama Monalisa, alipo itaji kumwonyesha mume wake, kuwa binti yao anajuwa kupika, akanunua Samaki wa baharini, na kumwambia Monalisa, wasaidiane kutengeneza wale Samaki, kwaajili ya baba yake.

Hakika lilikuwa nifumbuo la fumbo kubwa lililojificha kwa Monalisa, ambae ile kusogelea jikoni tu, akahisi kitu kinatoka tumboni, na kurudi mdomoni, hivyo akaziba mdomo wake haraka, na kukimbilia chooni, akimwacha mama yake anashangaa.

Dakika tano Monalisa anatoka bafuni, anaelekea tena jikoni, ambako anamkuta mama yake ametoa macho anamtazama, nae anaishia mlangoni, “mama siwezi kuingia jikoni, hao Samaki wanaarufu mbaya” alisema Monalisa, huku anaziba pua zake, kwa kutumia mkono wake wakulia.

“Mona, mbona awa Samaki wamenunuliwa leo, alafu arufu yao ya kawaida?” aliuliza mama Mona, ambae anamtazama binti yake, kwa macho ya udadisi, kichwani mwake akikumbuka miaka kumi na tisa nyuma, wakati alipo kuwa na ujauzito wa miezi mitatu.

“mbona arufu yao mbaya” anasema Monalisa huku anarudi sebuleni, “Khadijaaaaa” anaita mama Mona, “abeeee” aitika mwanamke aliekuwa nje ya nyumba upande wajikoni, huku anakuja mbio mbio.

“Khadija, niambie kila kitu, unamwonaje Mona, kwa siku za hivi karibuni?” aliuliza mama Mona, kwa sauti ya chini yenye ukali wa hali ya juu, huku amekazia macho Khadija, “yupo kawaida tu” alijibu Khadija, ambae ni dada wakazi, kwa kujiamini kabisa.

“Khadija, sitaki kugombana na wewe, naomba uniambie, unaona dalili gani za Mona, ulaji wake ata ushidaji wake hapa nyumbani” alisema mama Mona, kwa sauti ya chini ya ukali kama mwanzo.

Hapo Khadija nikama anagundua kitu, maana alitoa macho ya mshangao wa unga’amuzi, huku anamtazama boss wake, yani mama Mona, ambae pia anajiandaa kwa kupokea jibu, maana alisha juwa kuwa, Khadija amesha lipata jibu sahihi.

“kusema kweli mama Monalisa amebadirika kidogo, kwanza anapenda kujipikia, alafu anaweka rimao jingi kwenye mboga, na jingine anaramba, zaidi ya hapo uwa anashinda amelala chumbani kwambani kwake” hayo ndiyo maelezo ya Khadija kwa boss wake.

Hapo mama Mona anapandisha mikono kichwani, “mama yangu, nitaweka wapi sura yangu mimi, yani Mona amerudaia makosa yangu” alisema mama Mona huku anaegemea ukuta akijizuwia kuanguaka.

“vipi tena mama Mona, Mona amefanya kosa lipi kama lako?” wote walishtuliwa na sauti ya bwana Edson, ambae wakati huo, alikuwa anakuja jikoni, kuna jambo alikuwa anataka kuuliza kwa mke wake, na kwabahati mbaya, akakutia maongezi hayo.

“mume wangu, twende tukaongelee chumbani” alisema mama Mona, huku anaongoza sebuleni, “lakini mimi nilikuwa nataka kuage, kuna sehemu naenda kidogo, ila sitokaa ata kwa nusu saa” alisema bwana Edson, huku anamfwata Belinder aliekuwa anaongoza chumbani.

“sawa utaenda, ila naomba japo dakika tano, tuongee ili, naweza kufa kwa Bp” alisema mama Mona, huku wanaelekea chumbani, sauti hii, ilimfikia Monalisa, akiwa amesimama karibu na mlango wa chumbani kwake, akishangaa nini kinachoendelea.

Maana akujuwa kama jambo ilo linamuhusu yeye, au la, na kama inamhusu yeye ni jambo gani, ambalo yeye alifahamu, “au wanahisi naumwa sana, ndio maana mama ameshtuka sana” aliwaza Monalisa, ambae alikuwa bado ajihisi kichefu chefu, aliamua kuingia chumbani kwake, na kuchukuwa kipande cha limao juu ya meza yake ndogo, na kukilamba kidogo, kisha akapanda kitandani.

Naaaaaaam!, Belinder na mpenzi wake Edson, wanaingia chumbani, “mama Mona, unajuwa mimi ni mtu mzima, aitakiwi kushtuliwa, naweza kuwaacha yatima sasa hivi” alisema barozi Edson, ambae akuelewa nini kilikuwa kinaendelea.

“bora wewe mwanaume unaweza kuimiri, ujuwe mwenzio nimeona dalili za Mona kuwa ni mjamzito” alisema mama Monalisa, bila kusita sita, kisha kinafwata kimya kifupi, nikama bwana Edson anawaza jambo flani.

“baba Mona, mbona usemi chochote, nimekuwambia, Mona anadalili za ujauzito” alisema tena mama Monalisa, na hapo bwana Edson anashusha pumzi ndefu na nzito, kama ametoka kumbia mbio ndefu.

“hakuna namna limesha tokea, wacha nitulie, nitajuwa la kufanya, cha msingi mwache ajifungue salama, ataendelea na masomo” alisema mzee Edson, kwa sauti ya upole ya chini iliyo nyongea kidogo.

“hivi nimetumia kiswahili fasaha, au ujanielewa, ujauzito maana yake mimba baba Mona” alisema mama Mona kwa msisitizo, “nimekuelewa mama Mona, au unataka umpige mtoto, na kumfukuza nyumbani, kama wengine wanavyo fanya?” aliuliza bwana Edson barozi mstaafu, kwa sauti ya upole yenye ambayo iliashilia yakuwa, akutaka binti yake aumie kwa namna yoyote.

Mama Mona atoa macho kumtazama mzazi mwenzie, ambae ni sawa na mke wake, maana tayari uhusiano wao, uliwekwa wazi huyu kwa kila mtu, ata mke na watoto wake waliopo #Mbogo_Land, walisha juwa kuhusu Belinder na binti yake Monalisa.

“Mona ni binti yetu, na huyo mtoto ni mjukuu wetu” aliongea baba Mona, akionyesha wazi kuwa, anamaanisha anacho kisema, na siyo kwamba alikosea, anamfanya mama Mona, ambae alikuwa anawaza yak wake kichwani, yani mambo ambayo aliyapanga kuhusu binti yake.

“baba Mona, unajuwa ninamtoto mmoja, hivi ujuwa nina mpango gani na Mona, na leo amepata ujauzito, alafu wewe unazungumza kuhusu mjukuu” aliongea mama Mona kwa kulalamika.

“sasa mama Mona, shida ipo wapi, kama nikweli ni mjamzito, akuna la kufanya, maisha yataendelea” alisema bwana Edson, safari hii aliongea kwa sauti ya upole, nikama alihisi kuwa anaitaji busara kuliweka sawa ili swala.

“baba Mona, ujuwe maisha ya mtoto yanaaribika, anawezaje kuzaa akiwa amemaliza form four” alisema mama Mona, ambae alionyesha kuto kupendezwa kabisa, na kitendo cha binti yake kubeba ujauzito.

“mama Mona, ujauzito siyo kilema, wala tatizo, unakumbuka kipindikile, umebeba ujauzito wa Mona ilikuwaje?” aliuliza bwana Edson, “sawa baba Mona, lakini kumbuka nilikuwa na wewe na ulijuwa wajibu wako” alisema mama Mona.

“Basi ondoa shaka, mke wangu, Mona nae anao sisi, atuto mwacha binti yetu apate tabu, ata kama baba wa mtoto, atoweza kutoa huduma, naamini sisi tutaweza” alisema bwana Edson, ambae kiukweli aliongea kama siyo mzazi wa kiafrika.

Mama Mona anatulia kidogo anawaza, “acha kuwaza mama Mona, chakufanya we kaongee na Mona kwa utulivu, mwulize kuhusu huyo mwanaume ni nani, tabia hasiri na vingine ambavyo unaitaji kujuwa, mengine niachie mimi” alisema bwana Edson, kabla ajaondoka na kumwacha mke wake akiwa ametoa macho kwa mshangao.

Monalisa akiwa chumbani kwake, amejilaza kitandani, anawaza juu ya mshtuko wa mama yake kutokana na hali yake, mala mlango wa chumba chake ukafunguliwa, akaingia mama yake, akiwa mwenye uso ulio poa kiasi.

Monalisa anajiandaa kiakili, kukabiliana na mama yake, maana anajuwa kuna jambo linakuja mbele yake, anamwona mama yake anasimama kati kati ya chumba, na kutazama juu ya meza ndogo yenye mafuta na baadhi ya vipondose, anaona kipande cha limao, anakifwata na kukishika, anaokiona kimesha tumika. . . . . ENDELEA…….

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment