Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Inawezekana kuwaua wapiganaji, lakini mawazo yao hapana. ”- miaka 34 baada ya mauaji ya Guevara wa Afrika.
Thomas Isidore Noel Sankara alikuwa kamanda katika jeshi la Burkini, na Rais wa Burkina Faso mnamo kipindi cha (1983-1987).
Thomas Sankara alizaliwa mnamo Disemba 1949 kwa familia ya kikatholiki na alijiunga katika shule ya jeshi, kama babake, aliyekuwa mpiganaji katika jeshi la Ufaransa wakati wa Vita vya Dunia vya pili.
Sankara alikuwa kiongozi wa mapinduzi na mpiganaji ,aliyepinga kwa muda mrefu dhidi ya Ubeberu na kuepuka misaada ya kigeni, na misimamo na mipango yake ya mapinduzi iliyoimarisha hali ya kujitegemea kwa watu wake ,ndiyo iliyomfanya awe ishara kwa masikini wa Afrika.

mfumo wake wa ndani ulifanikiwa kuifanya Jamhuri ya Burkina Faso iwe nchi ya kwanza ya Kiafrika kufikia kujitegemea na kuwa na akiba ya ziada wakati huo, wakati ambapo alihimiza viwanda vya ndani, alihangaika kuinua kiwango cha maisha kwa wakulima, kuondoa ushuru uliokuwa ukiwaudhia, na kurekebisha ardhi, kwa hivyo uzalishaji wa ngano na pamba uliongezeka maradufu, lililofanya nchi ijitegemee na hata iwe na ziada ya kuuza nje.
Sankara alijali elimu kwa kiasi kikubwa, kampeni za kuondoa Ujinga kote nchini, kukuza afya ya umma kwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa uti wa mgongo, homa ya manjano na ugonjwa wa Surua, na alijali faili ya miundombinu na kuanzisha reli ili kuunganisha vijiji na miji, na kila kijiji kiwe na kliniki na shule.
Sankara pia alijali haki za wanawake na akawachagua wanawake bora zaidi katika nyadhifa kuu za serikali nchini, naye anazingatiwa kuwa Rais wa kwanza katika historia ya Afrika kuzuia kutahiriwa na ndoa za utotoni.
Ana neno maarufu juu ya haki ya wanawake akisema: “Mapinduzi na Uhuru wa wanawake huenda pamoja, basi hatuzungumzii Uhuru wa wanawake kama kitendo cha hisani au kwa upande wa huruma ya kibinadamu, bali haki za wanawake ni hitaji la msingi kwa ushindi wa mapinduzi, wanawake ni nusu ya anga”.
Alijulikana kama “Chi Guevara” kwa sababu ya kufanana kati yao katika haiba ya kibinafsi na ya kimapinduzi, upendo wao kwa maskini na kutatua kwa ajili yao na haki zao, mapambano yao dhidi ya Ubeberu na wafisadi, pamoja na kuwa wote wawili walianzisha mahakama za kimapinduzi kuhakimu wafisadi, kwa hivyo alisema katika hotuba juu ya kumbukumbu ya kifo cha “Guevara” na kabla Kuuawa kwake kwa muda mchache, “Guevara alikufa akiwa na umri wa miaka 39, nami sitaupitia”.
Na hivyo ilivyokuwa, sera yake ya mapinduzi na misimamo yake dhidi ya Ubeberu zilimfanya adui wa Ufaransa, kwa hivyo walipanga kumwua, na mnamo Oktoba 15, 1987, aliuawa na kundi lenye silaha lililompigia risasi wakati alipokuwa akienda kwenye mkutano mmoja na kumzika kwenye makaburi. Hii ilikuwa kupitia rafiki yake “Compaore” aliyewasiliana na taasisi za kigeni juu ya ulazima wa kumwua “Sankara” anayetisha masilahi yao,basi yeye ndiye aliyetamka ukweli bila hofa na kulipa maisha yake kwa hivyo.
Kesi ya Thomas Sankara nchni Burkina Faso: Ni nani aliyemuua Che Guevara wa Afrika?
Miaka thelathini na nne imepita tangu mauaji ya kushtua ya aliyekuwa rais wa Burkinafaso wakati huo Thomas Sankara yalipotokea, wanaume14 wanashitakiwa mahakamani, wakishutumiwa kushiriki katika mauaji ya mwanaume anayefahamika kama ” Che Guevara wa Afrika”.
Mwanaafrika huyo mwenye haiba kubwa alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa na umri wa miaka 37 katika mapinduzi ya tarehe 15 oktoba, 1987 yaliyomuweka madarakani rafiki yake wa karibu , Blaise Compaoré.
Miaka minne kabla, wawili hao walikuwa wamefanya mapinduzi yaliyomuweka madarakani Sankara kama rais.
Bw Compaoré ni miongoni mwa watu 14 wanaoshutumiwa kwa mauaji ya Sankara, lakini kwa sasa yuko uhamishoni katika nchi jirani ya Ivory Coast, ambako alitorokea baada ya kulazimishwa kujiuzulu wakati wa maandamano makubwa ya mwaka 2014.
Alikanusha mara kwa mara kuhusika katika kifo cha Sankara na amesusia kesi.
Licha ya kwamba kifo chake kilitokea miaka mingi, Sankara amesalia kuwa kielelezo kote Afrika huku picha zenye sura yake zikiendelea kuwekwa kwenye magari ya abiria kota Afrika magharibi, huku Afrika Kusini, kiongozi mwenye itikadi kali wa upinzani Julius Malema akimtaja kama mmoja wa watu wanaompa msukumo.
Ni kwanini Sankara anaonekana kama shujaa?
“Kwetu sisi, Sankara alikuwa mzaleno. Alipenda watu wake. Aliipenda nchi yake. Aliipenda Afrika. Alijitolea maisha yake kwa ajili yetu,” alisema Luc Damiba, katibu mkuu wa kamati ya makumbusho ya Thomas Sankara.
Ilikuwa ni chini ya utawala wake ambapo nchi ilipopewa jina upya – kutoka Upper Volta na kuitwa Burkina Faso, jina linalomaanisha “Ardhi ya watu wanyoofu”.
Sankara binafsi aliishi mtindo wa maisha ya kawaida. Alipunguza mshahara wake, na ule wa wafanyakazi wa umma. Pia alipiga marufuku matumizi ya madereva wa serikali na kuwazuia maafisa kusafiri daraja la kwanza wanaposafiri kwa ndege.
Elimu ilikuwa ni kipaumbele muhimu kwake-alipokuwa mamlakani, kiwango cha ujinga elimu kiliongezeka kutoka 13% katika mwaka 1983 hadi 73% katika mwaka wa 1987, na alisimamia kampeni kubwa ya chanjo.
Pia aligawa upya ardhi kutoka kwa mabwanyenye waliokuwa wanamiliki ardhi kubwa na kuwagawia moja kwa moja wakulima jammbo lililoongeza uzalishaji mkubwa sana wa zao la ngano nchini humo.

Sankara alitoa wito wa kuwepo kwa Umoja wa Afrika dhIdi ya kile alichokiita “ukoloni mamboleo” wa taasisi kama vile Shirika la fedha duniani (IMF) na Benki ya dunia.
Wakati mmoja alinukuliwa akisema: “Yule anayekulisha, anakudhibiti.”
Alifuata sera ya kupambana na ubeberu ambayo ilikosoa kutawala kwa Ufransa ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa katika nchi nyingi zilizokuwa koloni lake la zamani katika Afrika, kama vile Burkina Faso.
Mjane wake Mariam ameishutumu Ufaransa kwa kupanga mauaji yake.
Sanamu ya mita sita ya rangi ya shaba imesimama katika bustani ya kumbukumbu ya Thoamas Sankara katika mji mkuu Ouagadougou, ambayo ilizinduliwa mwaka 2019.

Wakosoaji wake wanasemaje?
Sera kali za Sankara za vuguvugu la kushoto zimekuwa zikikosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanayozitaka kama za kibabe.
Katika ripoti ya mwaka 1986 ya Amnesty InternatioAbdnal ilifichua madai ya wapinzani wake wa kisiasa waliofungwa na kuteswa vibaya.

“Ninadhani alichelewa sana kukubali wazo la demokrasia ya wengi na wale waliompinga hawakuzungumza naye na hawakusikika ,” alisema Serge Theophile Balima, ambaye alifanya kazi kama waziri wa habari katika serikali ya Sankara.
Profesa Balima aiongeza kuwa: ” Ukweli ni kwamba, walijipata wakitekeleza unyanyasaji ambao uliudharaulisha utawala wake.”
Ni kwanini kesi imechukua muda mrefu?
Mjane wake, lakini ilichukua miaka 15 kwa Mahakama ya juu zaidi kuamua kwamba uchunguzi unaweza kuendelea.
Hatahivyo, ni machache yamefanyika kuhusu kesi hiyo hadi Bw Compaoré alipopinduliwa katika mwaka 2014.
Mwaka uliofuatia, masalia ya mwili wake yalifufuliwa lakini tathini ya vinasaba DNA haikuweza kuthibitisha kuwa yalikuwa yake.

Katika mwaka 2016, Mamlaka za Burkina Faso ziliomba rasmi serikali ya Ufaransa kutoa nyaraka za kijeshi kuhusu mauji ya Sankara.
Nyaraka hizo za kumbukumbu ziliidhinishwa na kuhamishiwa nchini Burkina Faso katika awamu tatu – yamwisho ilikuwa ni katika mwezi Aprili 2021.
Ni nani mwingine aliyeshtakiwa?
Mkuu wa zamani wa majeshi wa Compaoré Jenerali Gilbert Diendéré na watu wengine 11 wanatarajiwa kuwa katika mahakama ya kijeshi. Wanakabiliwa na mashitaka ya ”kushambulia usalama wa taifa”, ” kushiriki katika mauaji” na “kuficha miili”.
Diendéré tayari yuko gerezani, baada ya kuhukumiwa kifongo cha miaka 20 kwa nafasi yake katika jaribio la mapinduzi ambalo halikufanikiwa katika mwaka 2015.
Kaka yake, Paul Sankara, alisema: “Tumesubiri kwa muda mrefu, kwa miaka 27 ya utawala wa Blaise Compaoré. Chini ya utawala wake hata tusingeota uwezekano wa kesi.”
Kaka yake, Paul Sankara, alisema: “Tumesubiri kwa muda mrefu, kwa miaka 27 ya utawala wa Blaise Compaoré. Chini ya utawala wake hata tusingeota uwezekano wa kesi.”

Miongoni kwa watu wanaoshutumiwa ni Diébré Jean Christophe, daktari aliyetengeneza cheti cha kifo cha Sankara, ambacho kilisema rais huyo wa zamnai alikufa kifo cha kawaida. Anashitakiwa kwa kugushi waraka wa umma.
Mwanume mwingine anayeshitakiwa bila kuwepo ni Hyacinthe Kafando, Mkuu wa zamani wa ulaslama wa Bw Compaoré’
Je kesi hii itakuwa na athari gani?
Kuna uoga kuwa kesi inaweza kuifanya Burkina Faso ambayo tayari inakabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya makundi ya jihadi yenye uhusiano al-Qaeda naq Islamic State kukosa uthabiti zaidi.
Bw Compaoré bado amebakia kuwa na ushawishi kwa kiasi kikubwa nchini humo na baadhi ya wachambuzi wametahadharisha kuwa baadhi ya wanajeshi ambao bado ni watiifu kwake wanaweza kusababisha matatizo.
“Siamini kwamba kesi ya aina hiyo inaweza kusababisha zaidi ukosefu wa usalama wa nchi ,” alisema Mathieu Pellerin, mchambuzi masuala ya Sahel katika taasisi ya International Crisis Group (ICG), alipohojiwa na Jarida la Ufaransa Jeune Afrique mwezi Aprili 2020.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.