Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba atajaribu kurejesha baadhi ya maeneo ya Ukraine wakati wa mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin Ijumaa ijayo.
Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba atajaribu kurejesha baadhi ya maeneo ya Ukraine wakati wa mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin Ijumaa ijayo.
“Urusi imechukua sehemu kubwa ya Ukraine. Wamechukua eneo muhimu. Tutajaribu kurudisha baadhi ya eneo hilo kwa Ukraine,” alisema katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya White House.
Trump na rais wa Urusi wameratibiwa kufanya mazungumzo huko Alaska wikendi hii. Trump amesema atajua ndani ya dakika mbili za mkutano wake na Putin ikiwa maendeleo yanaweza kupatikana.
Trump alielezea mkutano wa Ijumaa kama “mkutano wa uchunguzi” unaolenga kumtaka Putin kumaliza vita, akionyesha kwamba anauona mkutano huo kama mkutano wa awali tu.
Trump alionya tena kwamba kutakuwa na “mabadilishano na mabadiliko ya eneo” kati ya Urusi na Ukraine.
Hii si mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kutumia neno “kubadilishana maeneo,” ingawa bado haijafahamika ni eneo gani ambalo Urusi inaweza kukabidhi kwa Ukraine, hasa kwa vile Kyiv haijawahi kudai eneo lolote la Urusi.
Daktari mwenye umri wa miaka 70 ahukumiwa kwa kumbaka mwanamke hospitalini

Mahakama Kuu ya Anuradhapura nchini Sri Lanka imempata daktari mwenye umri wa miaka 70 na hatia ya kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 25, mama wa mtoto mmoja ambaye alikuwa amefika katika kituo cha matibabu ili kuondoa kitanzi cha uzazi ambacho kilikuwa kimepandikizwa mwilini mwake.
Hakimu aliamuru daktari mshtakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka kumi na tano jela kigumu na mam mlalamikaji alipwe fidia ya milioni moja na nusu.
Hakimu pia alimhukumu daktari kifungo cha miaka mitatu jela ikiwa atashindwa kulipa fidia hiyo.
Baada ya hukumu hiyo kutangazwa, Wakili wa mshitakiwa, Kalinga Ravindra, aliiambia mahakama kuwa ameshangazwa na hukumu hiyo.
Netanyahu: Tuko kwenye kilele cha kumaliza vita’ Gaza

Channel 14 iliripoti kuwa Waziri wa Ulinzi wa Israel Yisrael Katz atafanya mkutano na uongozi wa kijeshi wa Israel Alhamisi ijayo ili kujadili mipango ya operesheni ya kutwaa udhibiti wa mji wa Gaza, kama sehemu ya juhudi pana za kutatua tatizo la Hamas. Mkutano huo pia utajadili njia za kupunguza muda wa maandalizi hadi “wiki chache tu.”
Idhaa hiyo imenukuu chanzo cha usalama kikisema kuwa jeshi la Israel limejishughulisha kikamilifu katika kuandaa mipango hiyo katika siku za hivi karibuni na litatekeleza maagizo ya serikali.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Israel “iko ukingoni mwa kumaliza vita,” akibainisha kuwa juhudi zinalenga “kuondoa mabaki ya mhimili wa Iran na kuwaachilia mateka wote.”
Netanyahu alifichua, wakati wa hotuba yake aliyoitoa katika ufunguzi wa Jumba la Makumbusho la Knesset mjini Jerusalem, kwamba baraza la mawaziri la usalama, katika mkutano wake wa mwisho Ijumaa usiku, lilifanya “uamuzi wa kushangaza” wa kuiondoa Hamas, baada ya jeshi la Israel kuchukua udhibiti wa asilimia 70 ya Ukanda wa Gaza.
Alieleza kuwa jeshi lilipokea amri ya kuudhibiti mji wa Gaza, ambao aliutaja kuwa “mji mkuu wa ugaidi.”
Netanyahu aliweka “kanuni tano za kumaliza vita: kuivunja Hamas na silaha zake, kuwarudisha mateka wote, kuondoa kijeshi Ukanda wa Gaza, kuweka udhibiti wa usalama wa Israeli juu ya Ukanda huo, na kuanzisha utawala mbadala wa kiraia ambao hauko chini ya Hamas au Mamlaka ya Palestina.”
Pia alisisitiza kuwa Hamas “inakataa makubaliano yoyote” na inadai kujiondoa kabisa, ikiwa ni pamoja na kutoka kwenye ukanda wa Philadelphi, kuachiliwa kwa wanachama wake mashuhuri, na dhamana ya kuzuia jeshi kuanza tena mapigano. Alisema kwamba “hakuna serikali inayowajibika ingeweza kukubali hili,” na kwamba njia pekee ya kuwarudisha mateka ni “kuondoa Hamas.”
Kwa upande wake, Hamas mara kwa mara imekuwa ikimshutumu Netanyahu na serikali yake yenye msimamo mkali kwa kukataa makubaliano ya kusitisha mapigano na mazungumzo yaliyofuata, na kuhatarisha maisha ya wafungwa.
M23 inaishutumu Kinshasa kwa kujiandaa kwa vita vya wazi wazi

Vuguvugu la AFC/M23 limesema kuwa serikali ya Kinshasa inajiandaa kwa vita vya wazi “licha ya kuwa imetia saini kanuni za kumaliza vita”.
Katika taarifa, vuguvugu la M23 lilisema kuwa limeona “shughuli za kukusanya askari na vifaa” katika maeneo mbalimbali katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini.
Serikali ya Kinshasa haijazungumzia madai haya ya M23 ya kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
Wiki iliyopita, upande wa serikali pia ulishutumu M23 kwa kukiuka kanuni hizi kwa kufanya mashambulizi na mauaji ya raia, jambo ambalo upande wa M23 ulikanusha.
AFC/M23 inadai kuwa imeona harakati za askari na vifaa kutoka maeneo ya;
- Kindu akielekea Shabunda Kivu Kusini
- Kinshasa hadi Bujumbura nchini Burundi
- Wanatoka Kisangani hadi Walikale katika Kivu Kaskazini.
Kundi hilo pia linadai kuwa siku ya Jumapili meli mbili “zinazobeba vikosi vya serikali ya Kinshasa” ziliwasili Uvira huko Kivu Kusini kutoka Kalemie katika jimbo la Tanganyika.
BBC iliuliza serikali na pande za kijeshi kile walichosema kuhusu madai haya ya AFC/M23 ambayo “yanatatiza mchakato wa amani unaoendelea”, lakini hawajatoa maoni yao hadi sasa.
Wiki iliyopita, jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lilishutumu vuguvugu la M23 kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kufanya mashambulizi mbalimbali yakiwemo mauaji ya makumi ya raia huko Kivu Kusini.
Mwanariadha wa Italia afariki baada ya kuanguka kwenye Michezo ya Dunia

Mchezaji nyota wa Italia Mattia Debertolis amefariki dunia baada ya kuzimia wakati wa Michezo ya Dunia nchini China wiki iliyopita.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 alipatikana akiwa amepoteza fahamu na waandaaji wakati wa hafla ya uelekezaji wa shughuli za michezo hiyo siku ya Ijumaa iliyopita huko Chengdu.
Muitaliano huyo alikufa siku ya Jumanne – siku nne baada ya kuzimia.
“Licha ya kupata matibabu ya haraka ya kitaalam katika moja ya taasisi kuu za matibabu za Uchina, aliaga dunia,” waandaaji wa Michezo ya Dunia walisema katika taarifa.
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Uelekezaji (IOF) Tom Hollowell alisema “hakuwa na uwezo wa kuelezea vya kutosha kina cha huzuni mbaya kufuatia kifo hicho “.
Sababu za kifo cha Debertolis hazijulikani kwa wakati huu.
Michezo ya Dunia ni tukio la michezo mingi linalofanyika kila baada ya miaka minne kwa matukio ambayo hayajaorodheshwa katika Olimpiki.
Debertolis alikuwa akishiriki katika fainali ya tukio la umbali wa kati la wanaume, ambalo lilifanyika katika halijoto iliyozidi nyuzi joto 30, alipoanguka.
Uelekezaji ni mchezo wa nje ambapo washiriki wanapaswa kuvinjari kati ya vituo vya ukaguzi visivyo na alama kwa kutumia ramani.
Unahusisha mchanganyiko wa shughuli za kimwili na usomaji wa ramani na utatuzi wa matatizo.
Alikuwa sehemu ya timu ya taifa ya Italia na alimaliza akiwa wa tano katika fainali ya Kombe la Dunia la 2022.
Debertolis, ambaye alihitimu kama mhandisi wa ujenzi, aliishi Uswidi na alikuwa akisomea shahada ya uzamifu -PhD katika chuo kikuu huko Stockholm.
Waandaaji wa Michezo ya Dunia walisema “wataendelea kusaidia familia ya Debertolis kila njia iwezekanayo.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.