Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mali imewakamata makumi ya wanajeshi wanaoshukiwa kupanga njama ya kupindua serikali ya kijeshi, ambayo yenyewe ilichukua mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi katika mapinduzi.

Tangu kuchukua madaraka katika mapinduzi ya 2020 na 2021, jeshi limeendeleza ukandamizaji dhidi ya wakosoaji wake licha ya kuenea kwa utovu wa usalama kutokana na mashambulio ya wanajihadi.
Kwa siku tatu sasa, jeshi limeendeleza kamatakamata ambapo hadi sasa watu 20 wamekamatwa kwa mujibu wa vyanzo wa usalama nchini humo, wanajeshi wawili wakiripotiwa kukamatwa usiku wa jumapili kuamkia Jumatatu.
Miongoni mwa waliokamatwa ni jenerali Abass Dembele aliyewahi kuwa gavana katika eneo la Mopti ya kati na afisa wa jeshi anayeheshimika.
Tangu 2021, mali imekumbwa na mashamnbulio ya wanajihadi wanaohusishw a na kundi la al qaeda na Islamic tstae ambao wamekuwa wakiendeleza mashambulio katika eneo la sahel.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.