Sehemu ya pili.
Hivi leo iwapo nisingekua mwanahabari wa mwengoya,ningelikua mwanahabari wa runinga.Mwaka 2006 fursa mbili,zilibisha hodi mwenye tabasamu kujiunga na KTN kitengo cha habari za kiswahili Mkubwa Bwana Kizito Namulanda aliniarifu nilikua nimepokezwa jukwa,huku nilikua nimepata kazi na kituo Cha Radio na Runinga cha Imani,nilitafuta ushauri wa wazazi.Wao walipenda Radio Saana na hasa kituo hicho kipo karibu na nyumbani.Nilifunzwa na Babu yangu niwasikilize wazazi wangu niliwaridhisha .Mchango wao naukumbuka, mama alininunulia magazeti ya Nation,standard na taifa Leo kila siku mimi mwanawe nifikie ndoto yangu.Baba naye alininunulia santuri kucheza kwa kinanda Cha majira kuwa DJ,nikiwa mdogo na kunipa fursa kusikiliza radio,sikukaidi azma yao.Nilimpigia Mkubwa wangu Kizito Namulanda,nikamshukuru kwa fursa hiyo.Nilijiunga na Imani Radio nikatwikwa jukumu la kusimamia kitengo cha habari.Nikameza radio Hadi leo.Nimepititia mikono salama nikiwa KBC radio Taifa kitengo cha michezo,wakaning’oa magugu na kunisanifisha maji ya lugha sanifu.Mkubwa Jack Oyo Selvester,Ustadhi Peter Kimeu,Martin Kingasia,Omole Asiko na Salim Manga nilipatana chipukizi Cheye David,Isaac Lemoka,Dismas Otuke,Abwao ambaye tupo naye RMS, Loice Ligare Msyoki na Michael Were Muhusia bonga boli.Maisha ya mwanahabari yanaendelea.Nimepitia hapa studioni nione iwapo nisingekua mwanahabari wa Radio fursa iliyolala ya Runinga ningetokea vipi.Wacha nikushauri ndugu yangu usikate tamaa safarini wakati unapoandika kurasa za maisha yako,nikitabu kitasomwa siku moja.Upo vitani usife moyo.Jifunze kutokana na waliofanikiwa usia wake bwana Nzile aliniusia siku moja wikendi nilipomtembelea pale KTN nilipofikisha mkanda wa habari za Makamu Rais Awori,Ukiona vyangaa vimepitia changamoto.Hata wewe utafanikiwa cheza Kama wewe.Katika dunia ya Sasa kuna demokrasia na domokrasia usiwasikikize wanaotumia domokrasia kugandamiza demokrasia.Maana wapo miongoni mwetu kukatiza azma yako.Songea karibu na waliofanikiwa utafanikiwa.Nawashukuru wote walionilea kitaaluma Mchango wenu umeniweka mjini leo.Safari bado inaendelea.
Nashukuru kubonyeza kwenye tuvuti yangu cantonadigital.wordpress.com.
Wewe ni was maana sana. #GetInspired #Iposiku #CantonaJosephMotivates.

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.