Kuwa Makini na Watu hawa.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya watu ambao unatakiwa kuwa nao makini sana kwenye maisha yako ni wale ambao wanakuja KUKUPUNGUZIA KASI.

Hawa ni wale ambao, unapoamua kuanza kuendelea kwenye mwelekeo fulani tu…

…basi wanahusika kwa namna fulani KUKURUDISHA ULIKOTOKA.

Yaani, unaweza kuwa baada ya KUUMIA KIHISIA kwenye MAHUSIANO, umekaa chini na ukaamua “kumove”…

…basi wao ndio wanarudi tena, wanataka urudi ULIKOTOKA.

Ukiwa umeamua kuachana nao KIBIASHARA, pale unapotaka kuanza kufungua UKURASA MPYA…

…basi wao ndio huwa wanaanza kurudi kukuomba MUANZE UPYA tena, ila Ndani yao wanajua WATAKUACHA TENA NJIANI.

Mara nyingi, aina hii sio kwamba huwa ni MARA YA KWANZA, yaani ni KAWAIDA YAO.

Wakikuona unaanza kusonga tu, huwa wanarudi kwa KASI na wengine wanarudi kwa kutia HURUMA SANA.

Wengi wameshajua UDHAIFU WAKO na huwa wanatumia kama mbinu ya kukurudisha nyuma.

Ukijaribu kutathmini, utagundua kuwa kila wakati unashindwa kusonga mbele kwa SABABU YAO.

Ukiwagundua watu hawa, ni lazima ufanye UAMUZI MGUMU wa “Permanent Departure”.

Yaani fanya maamuzi na usirudi nyuma Kama kweli unataka KUVUKA HAPO.

UMECHOSHWA na hali uliyonayo?

Uko SERIOUS Unataka nikusaidie KUTIMIZA MALENGO YAKO?

Kama majibu yako ni NDIO

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment