Mambo Matatu Muhimu Ya Kuyatafari Ili Uwe Tofauti Na Wengine…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Chuo Ni Kiwanda

ii. Kozi unayosoma ni chaguo Lako?

iii. Katika Aina 6 Za UTAJIRI, Masomo Yako Yatakusaidia Kuupata Upi?

Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo La Kwanza

– Chuo Ni Kiwanda

Je, Wewe Ni Bidhaa Ipi Kati Ya Hizi?

Kila chuo ni kiwanda ambacho kinapokea malighafi na kutoa bidhaa.

Kama ilivyo kwa viwanda vingine, wako ambao wanaondoka chuoni wakiwa ni bidhaa nzuri sana na wengine wanaondoka wakiwa ni bidhaa zisizofaa kabisa.

Kuna watu ambao waliingia chuoni wakiwa watu wema sana na walitoka wakiwa wameharibika mno.

Wengine walipata maambukizi ya magonjwa wakiwa chuoni, wengine walipata uraibu (addiction) wakiwa chuoni.

Wengine walianza kuwa walezi wakiwa chuoni na pia wapo ambao walikatisha masomo kwa sababu ya ujauzito ambao hawakuutarajia wakiwa chuoni.

Kwa ufupi, kuna watu wengi ambao ndoto zao zilifia walipofika chuoni.

Kwa upande mwingine, kuna watu ambao chuo imekuwa ni baraka kubwa sana kwenye maisha yao.

Wapo ambao walibadilisha tabia na kuwa watu wema sana wakiwa chuoni.

Kuna watu walianza kumcha Mungu wakiwa chuoni, kuna watu walipata marafiki wazuri waliowasaidia kufanikiwa kwenye maisha yao wakiwa chuoni.

Kuna watu walianzisha biashara wakiwa chuoni na kuna watu walijitofautisha kabla hawajahitimu masomo yao na walikuwa tayari wameshapata nafasi za kazi.

Kwa kundi hili, chuo kwao imekuwa ni sehemu ya kubadilisha maisha yao na kuwapa mwelekeo wenye mafanikio makubwa.

Kama ungependa kuondoka chuoni ukiwa ni bidhaa nzuri, adimu na yenye kuhitajika, basi hakikisha umesoma kitabu hiki sura ya mwisho.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment