PAMOJA CHAN 2024: Licha ya Changamoto Nyumbani Sudan yapata Sare Mechi ya Kwanza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Sudan haijashuhudia mechi za ligi kuu kutokana na hali ya vita inayoendelea nchini humo, hali ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa maandalizi na utimamu wa wachezaji wake.

Timu ya taifa ya SUDAN
Timu ya taifa ya SUDAN © caf

Katika hali ya kusisimua na ya kipekee, timu ya taifa ya Sudan ilirejea uwanjani kwa mechi ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu cha sintofahamu ya kisiasa na kukosekana kwa ligi za ndani. Katika mechi yao ya kwanza ya Kundi D kwenye michuano ya PAMOJA CHAN 2024, Sudan walilazimishwa sare ya bila kufungana na Congo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Sudan haijashuhudia mechi za ligi kuu kutokana na hali ya vita inayoendelea nchini humo, hali ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa maandalizi na utimamu wa wachezaji wake.

Kocha Kwesi Appiah
Kocha Kwesi Appiah © caf

Kocha mkuu wa Sudan, James Kwesi Appiah, hakusita kueleza changamoto alizokumbana nazo:

“Kama nilivyosema hapo awali, inahusiana na nidhamu ya wachezaji wetu. Unaweza kusema kutoka uwanjani kuwa wachezaji hawako sawa kabisa, ukizingatia jinsi walivyocheza – mara kwa mara walikuwa na shida ya misuli na kuanguka chini pasipo na ulazima.”

Kwesi alisema kuwa timu hiyo ilikuwa na siku nne pekee za maandalizi kabla ya kuivaa Congo – muda usiotosha kuandaa kikosi cha ushindani.

“Katika soka, sio kile kinachotokea tu uwanjani. Inabidi ujaribu kuwaelekeza wachezaji wako kufanya zaidi ya matarajio yako. Nimekuwa na mikutano mingi ili kuwafanya wacheze kwa kiwango kile. Huwa ni ngumu unapokuwa na timu inayoenda kwenye mashindano bila hata wiki ya maandalizi – ni tatizo, lakini niliwapa motisha sana.”

Sudan sasa inajiandaa kwa mechi yao inayofuata dhidi ya Nigeria, huku kocha akieleza matumaini yake kuwa na muda wa kutosha kuhakikisha wachezaji wanapata utimamu wa mwili na umakini wa kiuchezaji.

Mashindano ya CHAN (African Nations Championship) yanashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee, na kwa mara ya kwanza yanafanyika katika ukanda wa Afrika Mashariki. Uwanja wa Amaan, Zanzibar, ni mwenyeji wa mechi za Kundi D.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment