Mambo Matatu ya Kukusaidia Kujua Biashara Inayokufaa…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Fanya biashara ambayo umejenga ujuzi nayo.

ii. Tafuta biashara ambayo unaweza ukaianza sasa hivi.

iii. Jiulize, una uwezo wa kuwafikia wateja katika biashara unayotaka kuifanya?

Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo la Tatu

– Jiulize, una uwezo wa kuwafikia wateja katika biashara unayotaka kuifanya?

Mimi ninapouza vitabu swali langu la kwanza ni, mteja wangu ni nani na ninawezaje kumfikia.

Kwa hiyo kabla hujaanzisha biashara yako jiulize, katika watu walionizunguka ni nani wanaweza kuwa wateja wako.

Ukiweza kujijibu swali hili basi hii ni ishara njema kwako.

Tambua kwamba hakuna maana ya kufanya biashara ikiwa huwezi kuuza au kufikia walengwa.

Uzuri wa biashara upo katika uwezo wako wa kufanya mauzo.

Lengo la biashara ni kupata faida, na faida ni matokeo ya wewe kuuza bidhaa.

Jitahidi kuchagua biashara ambayo unawajua wateja wake na una uhakika wa kuuza.

Vinginevyo biashara hiyo haikufai kabisa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment