Kanuni ambayo Imenisaidia.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja Kanuni niliyowahi kujifunza huko nyuma na ikanisaidia sana ni…

“USIJARIBU KUWASHUSHA WENGINE ILI WEWE UPANDE,WEKA BIDII NAFASI YAKO IPO”.

Kupitia Kanuni hii nilijifunza kuwa ni mara chache sana kusikia ndege zinagongana hewani ni kwa sababu…

…ukiamua kupandisha viwango vyako na Vikawa juu sana kuna nafasi ya kutosha tofauti na Ukiwa chini kama gari ambako msongamano ni mkubwa.

Kanuni hii niliipata wakati nasoma biblia (1 Sam 26) ambako Sauli alikuwa a namtafuta Daudi ili Amuue kwa kuhofia atachukua nafasi yake ya ufalme.

Daudi akiwa na Abishai walienda usiku hadi kambi ya sauli na mwanajeshi wa Daudi alipotaka kumuua Sauli akiwa katika Usingizi mzito Daudi alimkataza.

Badala yake alichukua Chupa yake ya Maji na kukata pindo la vazi lake ili kumuonesha baadaye kuwa alikuwa na nafasi ya kumdhuru lakini hakufanya hivyo.

Mara nyingi unaweza kujua udhaifu wa mshindani wako, unaweza kuweka nguvu kubwa kumuharibia sifa, kumzushia na hata kuandaa mbinu za kumdhuru.

Unachotakiwa kujua ni kuwa mbinu hizi huwa si za kudumu na hazitakufikisha unapotaka.

Kinachouma ni kuwa kadiri utakavyozitumia mwenzako ndio atazidi kufanikiwa zaidi kwani Mungu itabidi aingilie kati Kumtetea.

Ni muhimu kujua kuwa SI LAZIMA UMSHUSHE MWINGINE KWA HILA ili WEWE UPANDE.

Fanya bidii katika NAFASI YAKO ya sasa, WEKA MACHO yako katika KUJITOFAUTISHA na MAJIRA YAKO YATAKUJA.

Kumbuka MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

Wanauwezo wa kuchafua jina lako ila hawana uwezo wa kuondoa Neema ya Mungu iliyoko juu yako

Mke wa Potifa alifanikiwa kuchafua jina la Yusufu Nchi Nzima ila Mungu hakumruhusu mke wa Potifa aiondoe Neema iliyokuwa juu ya Yusufu.

Neema iliyokuwa juu ya Yusufu ilimwinua tena, ilimtambulisha tena, ilimketisha na wakuu tena, ilimpa jina la sifa tena mahali pale pale alipochafuliwa

Ninakuombea pamoja na kwamba wamechafua jina lako kama Mungu aliruhusu waone likichafuka, Mungu aruhusu pia waone likisafishwa tena

We nyamaza tu kimya nakwambia wataona Neema ya Mungu ikikwinua tena, wataona Neema ya Mungu ikikuketisha na wakuu tena, wamechafua jina lako ila hawajaondoa Neema ya Mungu juu yako

Acha Neema ikakuinue na kukutambulisha tena katika jina la Yesu.

Umeshakutana na mtu anayejaribu kumshusha mwingine kwa mbinu Chafu?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment