UNAPOPITIA KWENYE HALI NGUMU UWE MAKINI NA MAKUNDI HAYA (5) YA WATU.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

1) Kuna watu ambao ukiwaambia changamoto yako kwa undani, wataitumia “kutake advantage”, wanajua KIHISIA uko DHAIFU hivyo watataka kutumia fursa hiyo KUPATA WANACHOTAKA kutoka kwako.

2) Kuna ambao watatumiwa na WATESI wako kuja kujifanya kukuletea MSAADA kumbe ni wajumbe wa uovu wanaopeleka taarifa kwa wale waliopanga au wanaofurahia mateso yako.

3) Kuna ambao walikuwa wanatamani sana ANGUKO lako kwa MUDA MREFU. Watakaposikia unapitia hali NGUMU ni HABARI NJEMA kwao. Hawa watasambaza kwa KASI sana habari zako mbaya ili wazidi kukuumiza.

4) Kuna ambao MAPITO yako ni UJUMBE WAO kwako wa kukukosoa Kuhusu ULICHOAMINI au ULICHOSIMAMIA hapo mwanzo. Ni kama wanasema, “Kiko wapi sasa..”. Hawa wanatamani hali yako iendelee zaidi.

5) Wale ambao walitamani UWE CHINI ya HIMAYA na MAMLAKA YAO. Wakisikia au Kuona Uko kwenye MAGUMU wanataka kuyatumia ili UKUBALIANE nao MATAKWA yao ya MUDA MREFU ambayo ulikuwa UNAYAKATAA.

N:B USIRUHUSU hali NGUMU ikufanye UMUAMINI kila MTU kwa HARAKA na UFUNGUKE kwa YEYOTE YULE. Pata UTULIVU na JITAHIDI sana KUSIKILIZA MOYO WAKO.

Ukiona UNASITA KUMSHIRIKISHA MTU fulani, hata kama anaonekana anaweza kusaidia ila moyo wako unagoma, usimwambie.

NAKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE AKUEPUSHE NA WATU WA AINA HIZI TANO.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment