Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Usijiingize kwenye mawazo ya jumla (Avoid Mass-Thinking)
ii. Fanya kitu kimkakati.
iii. Unaweza kuunda kitu kipya kwenye kipindi hiki cha janga
iv. Tafuta hekima ya kiMungu
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina Ya Kwanza
– Usijiingize kwenye mawazo ya jumla
Janga huwa lina tabia ya kutengeneza kile ambacho kinaitwa fikra za wengi.
Waliowengi huwa wanakuwa wanafikiria kwenye mwelekeo mmoja…
…kwa sababu kwenye kipindi cha janga watu huwa hawapati muda wa kufikiri.
Namna hiyo ya kufikiria huitwa “fikra za kundi”.
Fikra hii hufafanuliwa kama hali ya kisaikolojia ambayo inatokea kwenye kundi la watu.
Ambapo mawazo yao huelekea upande mmoja bila kupata muda mzuri wa kufikiri.
Na hiyo hupelekea maamuzi yasiyo na tija.
Kumbuka kuwa sio kwamba watu huwa hawapati muda wa kufikiri tu.
Ila pia kutokana na changamoto zinazowakabilia…
…huwa wanachoka pia kufikiri kuhusu chochote na wanaweza pia kukataa kufikiri.
Kwenye hatua hii hitaji ni kile ambacho kisipokuwepo hutaweza kuishi.
Tamanio ni kile ambacho kinakufanya ujisikie vizuri.
Kinakufanya ujisikie raha ijapokuwa unaweza kuishi bila kuwa nacho.
Wakati wa janga hutakiwi kununua kila kitu lazima uwe makini kuhusu gharama.
Punguza matumizi kwenye kila kitu isipokuwa…
…kwenye kile tu ambacho kinakuletea fedha.
Kuwa mwangalifu kujua kila mahali pesa yako inakoenda.
Na utahitaji kubadili mfumo wa matumizi ya muhimu.
Kama vile kiwango cha vocha kwa ajili ya internet.
Vocha kwa ajili ya mawasiliano ya kawaida, nguo, n.k.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.