Unapofwatilia Ndoto yako….

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Miaka Mingi iliyopita mwana alizaliwa katika familia ya Mzee Benjamin Endesha SR na mwenda zake Queen Elizabeth Endesha General -Wazazi walinipa makuzi ya kuwa mwanahabari-Katika familia jamaa wa mbali katika familia yetu Eda Adede jirani yetu alikuwa mwana habari kipindi nakua alikua anatangaza shirika la serikali nchini Kenya KBC-siku moja mama akanishauri kufwatilia ndoto hii-Nashukuru kwa jitihada za mama mzazi- Baba mzazi alipenda redio na alinpa mda kusikiliza radio za kimataifa na Tanzania.Siku moja,miaka 22 iliyopita, nikiwa natafakari alfajiri sana kipindi ambacho maisha yangu yalikuwa yamevurugika sana na ndoto zangu zikionekana haziwezi kutimia tena…

Kipindi ambacho niliamka asubuhi nikiwa nachangamoto lukuki kufukuzia ndoto zangu.

Baada ya kuamka nilianza kumuomba Mungu na maneno yangu ya kwanza yakawa…

“Nakushukuru Mungu kwa kuamka salama, ila leo NIMEFANYA MAAMUZI kuwa nitaishi kawaida na sitaendelea tena na kufuatilia NDOTO HII”.

Ghafla machozi yalianza kunitiririka na nikasikia sauti iliyoniimarisha moyoni ikisema…

“Usifanye MAAMUZI kulingana na HALI YAKO ya SASA bali fanya MAAMUZI kulingana na NDOTO yako”.

Ni wazi nilijua haikuwa sauti yangu, niliamua kujibu na kusema…

“NITAJARIBU TENA, NITACHUKUA HATUA, Sitakata TAMAA”.

Siku hiyo niliamua kujilazimisha kutoka nje na kwenda kumtembelea rafiki yangu na tuliyoongea yalinitia moyo zaidi kuendelea na safari.Safari ya bamba ni machero.

Kuna wakati UNACHOKIONA MOYONI kitatofautiana na UNACHOKIPITIA KWENYE UHALISIA MAISHANI.

Nyakati hizi zinaweza kukujaribu UFANYE MAAMUZI ya kukata TAMAA na KUACHA kufuatilia NDOTO na MALENGO YAKO.

.

Nilichogundua HALI kama hii ni MCHAKATO ambao lazima uupitie na HAUTAUPITIA MARA MOJA.

Kila unapotaka kubadilisha kiwango kimoja kwenda kingine UTALAZIMIKA kuvuka hali ya namna hii kwa USHINDI.

Zimekuja nyingi za NAMNA HIYO ila kila wakati nimekumbuka “HUWEZI KUIISHI NDOTO YAKO kwa KUKATA TAMAA na KUIKIMBIA”.

Bila kujali leo kuna kitu kipi unapitia kuhusiana na NDOTO na MALENGO YAKO naomba uisikilize sauti hii na kuiamini –

“USIFANYE MAAMUZI kulingana na HALI YAKO ya SASA bali fanya maamuzi kulingana na NDOTO

YAKO”.

Utang’atwa sana utalia sana lakini hakikisha asali hauitupi chini.Safari ya bamba ni machero.

Hatua kwa hatua usidharau mwanzo mdogo pichani miaka mingi sana iliyopita………..

Maisha sio jinsi ulivyo leo bali jinsi unavyo jiona kesho maana pale unapojiona kesho ndio panatia hamasa namna ya kuishi leo. Asiye jiona kokote kesho hana lolote hata leo.

Mama yangu alipenda uandishi alinichochea kusoma magazeti alipenda uanndishi wa Ken Walibora sasa marehemu.Nilikuenzi na kusoma Riwaya ya Siku Njema,nilitahiniwa kidato cha nne kitabu chako,nikakipenda kiswahili,tokea hapo. Nilifwatilia Maisha yako. Hadi ukawa mtu niliyemuiga ( role model),ulikua mkereketwa wa kiswahili mtoto wa mwalimu. Jirani wetu,mtoto wa nyumbani Makutano kwa ngozi, Cherangany. Ulilea wengi nikiwa mmoja wao.Ulikerwa na watu walioboronga kiswahili,ulisema tukubali kukosolewa. Kweli duniani twapita mfano umande asubui.

Kumbukizi zimenijia mtu aliyependwa kwa usanifu wa kiswahili.Kazi zako zitadumu,mwandishi na mtangazaji Hafi anadumu kupitia kazi zake.
Mama angu Marehemu alipenda ualimu na usanifu wa kiswahili ,mwenda zake Queen Elizabeth Endesha (General) akanishauri kufwata nyezo zako za kuwa mwandishi wa vitabu na mtangazaji.

Get up.

I didn’t know how many people would need to hear it. I didn’t know how often I’d need to hear it myself.

This is your reminder that no matter how long you’ve been down, you can get up again. Stand tall again. Try again. Love again. Live again. Get up again.
God of the mountain He is God in the valley.Make that leap step today.

Umeshawahi kupitia hali kama hii?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment