Mikakati 4 Ya Kufanya Katika Kuboresha Uongozi Wako Wakati Wa Majanga…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Chagua watu wenye akili na wenye vipaji vya kipekee

ii. Vunja Mtazamo wa kibaguzi

iii. Uhitaji wa kusimamishwa kwa urasimu

iv. Uhitaji wa kuona mbele

Katika Makala Hii Tutazungumzia Mkakati Wa Nne

– Uhitaji Wa Kuona Mbele

Kila mtu wa kawaida anafikiria kuhusu athari ya janga ndani ya…

…kipindi ambacho linatokea, lakini viongozi wanafikiri zaidi ya hapo.

Vitu vingi sana vitaathiriwa kutokana na janga.

Viongozi inatakiwa wafikirie, wachambue, wagundue na kutengeneza mpango kazi…

…wa namna ambayo wataweza kuendelea kuishi baada ya janga.

Wakati kila mmoja atakapokuwa anasherehekea kuisha kwa janga…

…viongozi watatakiwa kujiandaa na matukio ya baadae ya janga.

Kitu cha kukumbuka, janga huwa linakuwepo kwa muda mfupi…

…lakini athari yake huwa inadumu kwa muda mrefu kwenye maeneo mbalimbali.

Kazi ya kiongozi ni kutarajia athari za janga kibinafsi…

…kitaasisi na kimfumo na kuunda njia ya kimkakati wa namna ya kulishughulikia.

Ni vyema kukumbuka kwamba, unaweza kuwa na watu madarakani lakini wasiwe na jawabu la matatizo.

Jawabu inatakiwa litoke kwa watu walioko nje ya mfumo wa watu wako wa karibu.

Usijizuie kufanya kazi na watu wapya! Kuna watu ambao wataibuka na kung’aa kwenye eneo lako kipindi cha janga.

Badala ya kupambana nao, tafuta namna ya kuwafanya sehemu ya jawabu lako na…

…pale inapobidi wafanye kuwa sehemu ya watu wako wa karibu.

Kumbuka, kila kiongozi ambaye alipambana na watu wapya wanaoibuka washindi kwa sababu ya…

…uwezo wao wa kutoa majibu wakati wa janga, aliishia kupoteza ushawishi wake, nguvu yake na nafasi yake.

Kuwa na akili!

Usimfanye kila anayeibuka mshindi wakati wa janga awe adui yako badala yake…

…uwe mwenye akili kuwafanya sehemu ya kutengeneza jawabu lako.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment