Nikasikia sauti ikiniambia

Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu nilipokuwa katika kutafakari na maombi nikaona watu walio katika bonde la machozi na vilio na hata alipotokea wa kuwafariji walikataa kufarijika

Nikasikia sauti ikiniambia tazama,nikataza mabakuri yamejaa machozi ya wale waliokuwa wakilia kwasababu ya mapito na mateso na taabu wanazozipitia

Ndio nikasikia sauti ikiniambia tazama nikatazama tena nikaona malaika akija na mkate na maji akawapa wale watu wakala na kunywa gafla wakaanza kucheka na nyuso zao hazikuonekana na kilio tena

Ndipo nikapewa mistari hii

Mwanzo 21:6:7
Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.
Akasema, N?nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.

Mpendwa wangu acha Mungu akakufanyie kicheko na kila atakaesikia atacheka pamoja na wewe

Acha Mungu ninaemtumikia usiku na mchana akutoe kwenye hilo bonde la mauti na kilio sasa yatosha ulivyolia nimekuombea Mungu aliyemkumbuka Sara akukumbuke na wewe.

Kama unaamini comment “Bwana ninaomba unikumbuke nitoe katika hili bonde la kilio na mateso nifanyie kicheko” na itakuwa

Kisha fanyika baraka na kwa wengine kwa kushare ujumbe huu na Mungu atakubariki sana.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment