Iran yakutana na wanadiplomasia wa Ulaya kwa mazungumzo mapya ya nyuklia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g
Maelezo ya picha,Mazungumzo ya nyuklia yalifanyika katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Istanbul, Uturuki

Wanadiplomasia wa Iran wamekutana na wenzao kutoka Uingereza, Ujerumani na Ufaransa kwa mazungumzo ya nyuklia, kwa mara ya kwanza tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi kwenye vituo vya nyuklia vya Iran mwezi Juni.

Mashambulizi hayo yalizua vita vya siku 12, ambavyo pia vilipelekea Marekani kuyashambulia kwa mabomu maeneo kadhaa ya nyuklia ya Iran, na kupelekea mazungumzo ya nyuklia ya Marekani na Iran kumalizika ghafla.

Mataifa matatu yenye nguvu ya Ulaya yaliyohudhuria mazungumzo hayo yanayojulikana kwa jina la E3, yametishia kuiwekea tena vikwazo Iran ikiwa hakuna maendeleo yatakayopatikana katika mazungumzo ya mapatano mapya ya nyuklia ifikapo mwishoni mwa Agosti.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Kazem Gharibabadi alisema walifanya mjadala “mzito, wa wazi na wa kina”, na kukubaliana kuendelea na mashauriano.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment