Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiongozi wa Thailand amesema kuwa mapigano makali kati ya Thailand na Cambodia, ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 16 na maelfu ya wengine kuyahama makazi yao, yanaweza “kuelekea kwenye vita”.
Onyo la Kaimu Waziri Mkuu Phumtham Wechayachai linakuja wakati mapigano katika mpaka unaozozaniwa yakiingia siku ya pili, na hivyo kuashiria kuongezeka kwa mzozo huo ambao ulianza zaidi ya karne moja.
Nchini Thailand, mapigano katika majimbo ya Ubon Ratchathani na Surin yalijeruhi makumi na kusababisha zaidi ya raia 100,000 kuyahama makazi yao. Baadhi ya familia 1,500 katika jimbo la Oddar Meanchey nchini Cambodia zimehamishwa.
Viongozi wa dunia wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.