⏺Kuna wakati katika maisha,yoote uliyoyategemea hayaonekani kama yatatokea tena na woote uliowategemea wamekukimbia na kukuacha
⏺Katika kipindi cha namna hii unaweza kuwa na kitanda kizuri lakini kisikupe usingizi kwasababu ya maumivu ya moyo kutokana na mambo uliyokutana nayo ambayo hukuyategemea
⏺Najua naongea na mtu hakuna kinachoonekana kukupa tumaini kwenye maisha yako na umefika mahali moyoni una maumivu na uchungu usioelezeka
⏺Ile furaha ya maisha imepotea gafla kama mshumaa,na zile nguvu za kuendelea mbele gafla zimepotea ndani ya mifupa yako hujisikii tena kuendelea na chochote
⏺Na ule mwanga uliokuwa unauona gafla umezimika na giza nene limetanda mbele yako huoni tena pakupita,mawimbi ni mengi sana yaliyotanda mbele yako
⏺Hata Mungu uliyemtegemea kwamba angekusaidia ni kama na yeye amenyemanza gafla umejikuta huna tena msaada
⏺Nikiwa katika maombi nikasikia roho mtakatifu akiniambia mtie moyo huyu dada mwambie safari yako haiwezi kuishia hapa
⏺Nikasikia tena sauti ikiniambia mtie moyo huyu mama mwambie ndoa yako haiwezi kufia hapa bado lipo tumaini
⏺Nikasikia tena sauti ikiniambia mtie moyo huyu Baba mwambie akili za mwanadamu zinapoishia ndipo Mungu anapoanzia atafanya
⏺Mpendwa ninakuombea mpaka uvuke ng’ambo na ninakuhakikishia ya kwamba yeye aliyewavusha wana wa Israel wakavuka ng’ambo ya bahari ya shamu atakuvusha na wewe pia hatakuacha
Usilie tena mpendwa wangu jivike nguvu kwa upya, anza tena,jaribu tena utavuka ng’ambo
Kama unaamini comment “Bwana umetenda kwa wengi tenda na kwangu nivushe katika hili maana nakutegemea wewe tu” na itakuwa katika jina la Yesu
Kisha fanyika baraka kwa wengine kwa kushare ujumbe huu na Mungu atakubariki sana
Nawapenda na ninawaombea lazima tutavuka tu
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.