Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wanajeshi wa Cambodia na Thailand wanafyatuliana risasi tangu asubuhi katika eneo la mpakani linalozozaniwa.
Pande zote mbili zimeshtumiana kwa kufyatua risasi ya kwanza.
Hii inafuatia uamuzi wa Thailand kumfukuza balozi wa Cambodia na kumwita balozi wake kutoka Phnom Penh baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu la ardhini uliomjeruhi mwanajeshi wa Thailand kando ya mpaka.
Kwa mujibu wa jeshi la Thailand, wanajeshi wao walifyatua risasi baada ya kukabiliana na kundi la wanajeshi wa Cambodia waliokuwa na silaha kwenye mpaka unaozozaniwa huku Wacambodia wakisema ni Wathailand ambao walifyatua silaha zao kwanza.
Sasa, wanakijiji katika eneo la mpakani mwa Thailand wameagizwa kuhama.
Hadi kufikia sasa, hakuna nchi inayoonekana kuwa tayari kurudi nyuma.
Lakini mzozo huu ulianza mwezi uliopita, baada ya mzee wa Cambodia, Hun Sen, kumwaibisha Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra kwa kuvujisha mazungumzo ya simu kati yao kuhusu mpaka unaozozaniwa.
Hakuna anayejua kwa nini aliamua kufanya hivi.
Paetongtarn Shinawatra alisimamishwa kazi kama waziri mkuu na mahakama ya kikatiba nchini Thailand na serikali yake isiyopendwa na watu wengi haiwezi kumudu kuonyesha udhaifu wowote sasa katika kukabiliana na Cambodia.
Matokeo yake yamekuwa ni kuongezeka kwa vita vya maneno kati ya nchi hizo mbili, kusambaratika kwa biashara ya mpakani ambayo ina thamani ya mabilioni ya dola, na kuongezeka kwa hatari ya mapigano makubwa zaidi kati ya majeshi yao mawili.

Ubalozi wa Thailand watoa wito kwa raia kuondoka Cambodia
Wakati huo huo, ubalozi wa Thailand mjini Phnom Penh unawataka raia wa Thailand kuondoka nchini Cambodia kutokana na mapigano ya mpakani.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa Facebook, ubalozi ulisema kwamba raia wa Thailand walioko Cambodia wanapaswa kuondoka “mara moja” labda wawe na sababu za dharura za kuendelea kuwa huko.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.