Zaidi ya mashirika 100 ya misaada yanasema ‘baa la njaa’ linaenea kote Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Zaidi ya mashirika 100 ya kutoa misaada, ikiwa ni pamoja na Save the Children na Médecins Sans Frontières, yametoa taarifa ya pamoja “ya kutisha” juu ya kile wanachosema ni “baa la njaa kubwa” kote Gaza.

“Wapalestina wamejipata katikati ya matumaini na huzuni, wakingojea usaidizi na kusitishwa kwa mapigano, lakini badala yake wanaamkia hali mbaya inayozidi kuzorota,” inasema taarifa hiyo.

Israel imekiri kupungua kwa kiasi kikubwa cha misaada inayowafikia raia wa Gaza. Lakini maafisa wake wanasema chakula hicho kipo – na badala yake wakaelekeza kidole cha lawama kwa mashirika ya kutoa misaada kwa kushindwa kufikisha chakula hicho kwa raia.

Kwa upande wao, mashirika ya misaada kwa muda mrefu yameripoti changamoto za kuratibu njia salama na Israel za kusambaza misaada.

Katika siku za hivi karibuni, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imeripoti makumi ya vifo vya hivi majuzi kutokana na utapiamlo, huku mashirika hayo yakisema mamia ya watu wameuawa wakitafuta msaada katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment