Zaidi ya makundi 100 ya misaada yatahadharisha kuhusu njaa kali huko Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wakazi wa Gaza wanategemea misaada ya kibinadamu kuishi

Zaidi ya mashirika 100 ya misaada ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaonya juu ya njaa kubwa huko Gaza na kushinikiza serikali kuchukua hatua.

Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), Save the Children na Oxfam ni miongoni mwa waliotia saini taarifa ya pamoja inayosema wenzao na watu wanaowahudumia “wanadhoofika”.

Yanatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja, kufunguliwa kwa vivuko vyote vya mpaka, na mtiririko huru wa misaada unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Israel, ambayo inadhibiti uingiaji wa vifaa vyote Gaza, inakanusha kuhusika na uhaba mkubwa wa chakula.

Hatua hii inakuja siku moja baada ya wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas kusema watu 33, wakiwemo watoto 12, wamefariki kutokana na athari za utapiamlo tangu Jumapili.

Umoja wa Mataifa pia uliripoti kuwa hospitali zililaza watu katika hali ya uchovu mkali uliosababishwa na ukosefu wa chakula, na kwamba wengine walisemekana kuanguka mitaani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment