Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mke wa mshambuliaji wa Liverpool Diogo Jota ameadhimisha mwezi wa kwanza wa ndoa yao, wiki tatu baada ya Jota kufariki katika ajali ya gari.
Rute Cardoso aliweka picha za harusi yao iliyofanyika Juni 22, katika akaunti yake ya Instagram.
Picha tatu ziliambatanishwa na maneno “mwezi mmoja wa ‘hadi kifo kitakapotutenganisha,” na kuongeza kuwa “ni wangu milele”.
Jota, 28, alifariki dunia tarehe 3 Julai wakati gari aina ya Lamborghini alilokuwa akisafiria na mdogo wake, Andre Silva, lilipotoka tairi likapinduka na kuwaka moto huko Cernadilla katika jimbo la Zamora nchini Uhispania.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.