Zaidi ya watu milioni 1.5 wako katika hatari ya utapiamlo mkali, IPC yaonya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Foleni ya kupata chakula

Wataalamu wameonya kwamba zaidi ya watu milioni 1.5 huko Gaza, theluthi mbili ya wakazi wako katika hatari ya utapiamlo mkali au njaa hadi mwezi Oktoba.

Katika ripoti ya hivi karibuni, IPC, shirika ambalo linajishughulisha na usalama wa chakula duniani linasema “bidhaa zinazohitajika kwa ajili ya maisha ya watu zinapungua au zinatarajiwa kuisha katika wiki zijazo”.

Takribani watu 500,000 wanaripotiwa kukabiliwa na “janga”, hali mbaya zaidi kuripotiwa na IPC.

Onyo hilo linakuja wakati shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Kipalestina, Unrwa, likisema lina zaidi ya miezi mitatu ya chakula kwa wakazi wa Gaza “kilichorundikwa kwenye maghala” nje kidogo ya mpaka wa Israel.

“Mateso huko Gaza yamefanywa na binadamu na lazima yakomeshwe,” UNRWA inaongeza.

Kauli ya shirika hilo inajiri saa chache baada ya wizara ya afya ya Gaza kusema watu 19 wamefariki kwa njaa katika muda wa saa 24 zilizopita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment