Umewahi kuwaza gharama (price) ya kukombolewa/kuvunja maagano (hasa ya vizazi) ilivyo ngumu kuilipa mwenyewe? Fikiria yafuatayo.
Je! Unajua walioyaingia maagano hayo na miungu waligharamia kiasi gani? Mali, pesa, vitu, uhai, damu nk
Unajua yana umbali wa vizazi vingapi?
Unajua yana makubaliano mangapi? Ambayo yametimia na yasiyotimia. Je! Ukiambiwa sababu ya kuvunja kulingana na makubaliano, unaweza kuwa NAyo na ikawa na mashiko?
FIKIRI TENA
Je! Ni kweli sadaka unayotoa inatosha kuvunja makubaliano/maagano hayo?
KAMA HAITOSHI UNAHISI UTALIPA KIASI GANI MPAKA UWE HURU DHIDI YA VIFUNGO NDANI YA MKATABA? JE! KAMA HATA CHANZO CHA HAYO MALIPO NI SEHEMU YA MATOKEO YA MAAGANO UNAFANYAJE?
Unahisi masharti ya kuvunja unayofundishwa kila siku yaliyo bebwa kwenye juhudi zako binafsi/ vitu/ na sadaka yanatosha kukuweka huru?
UPANDE WANGU KILA NIKIWAZA HIVI HUWA NAIONA SABABU YA YESU KUJA KULIPIA DAMU YAKE KWA AJILI YA AGANO BORA ZAIDI. Hebu tuipe nafasi damu hii safi isiyo na hatia wala mawaa kutulipia kuliko kudhani tunaweza kujikomboa kwa vitu vyetu vinavyoshikika, na kuhesabika. KUFANYA HIVYO TUNAISHUSHA SANA THAMANI DAMU YA UKOMBOZI ILIYOMWAGA KWA AJILI YETU.
Kumbuka alienda msalabani kama Mwanakondoo lakini alifufuka kama Kuhani Mkuu. TAFAKARI
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.