Siku utakayoanza kujiona wewe ni zaidi ya wote kwenye kazi yako, huduma yako, kipawa chako na maisha yako… NDIO ITAKUWA MWANZO MDOGO WA MWISHO WAKO.
Huwezi mzuia njiwa asipite juu ya kichwa chako, lakini unaweza mzuia asijenge kiota juu ya kichwa chako.
Mawazo mabovu yaweza pita kichwani mwako lakini kamwe usiyaruhusu yakae maana yatakuchafulia maisha yako.
Anayekuambia usiseme uliyogundua au aliyokuambia, hakukatazi kwa faida yako Bali kwa faida yake mwenyewe.
Mengine ukisema ndio unapona, kwa sababu ukweli usiosemwa unaumiza zaidi kuliko unaosemwa. PAMOJA NA YOTE CHAGUA CHA KUSEMA USIJEJUTIA MDOMO WAKO. “Tafakari kutoka kalantini ya hiari”
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.