Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Usisahau kuwa kupenda ni HISIA Ila kuhitaji ni UHALISIA.
Kwa maneno mengine ni kuwa, usijichanganye kwenye maisha ukawakumbatia unaowapenda peke yao na ukasahau unaowahitaji.
Labda niseme hivi; unapougua ugonjwa na unahitaji matibabu, UNAMUHITAJI Daktari.
Hata Kama atakuwa na rangi, urefu au kabila ambalo haulipendi, Ila kwa wakati huo UNAMUHITAJI.
Watu wengi kwenye maisha yao, huwa wanashindwa kutimiza baadhi ya MALENGO kwa sababu wanatumia muda na nguvu nyingi kwa wanaowapenda na KUWAPUUZA wanaowahitaji.
Kila MAJIRA ya maisha yako kuna watu UNAOWAHITAJI.
Hata kama hauwapendi Ila hakikisha unawapa fursa ya kuchangia HATUA YAKO inayofuata.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.