Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Israel inasema imewashambulia kwa mabomu wanajeshi wa serikali ya Syria karibu na Suweida, walipokuwa wakiingia katika mji wenye wakazi wengi wa Druze kufuatia siku mbili za mapigano mabaya ya kidini.
Takriban watu 200 wameuawa tangu mapigano kati ya wanamgambo wa Druze na makabila ya Bedouin yalipozuka siku ya Jumapili, kundi la waangalizi lenye makao yake makuu nchini Uingereza la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR), liliripoti.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema ameamuru mashambulizi dhidi ya vikosi na silaha katika eneo la Suweida kwa sababu serikali “ilinuia kuzitumia dhidi ya Druze”.
Syria imelaani kuhusika kwa Israel na kusema mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wanajeshi na raia.
Hii ni mara ya kwanza kwa vikosi vya serikali ya Syria kutumwa Suweida tangu waasi wanaoongozwa na Waislam walipompindua Rais Bashar al-Assad mwezi Disemba.
Jamii nyingi za wachache – ikiwa ni pamoja na Druze, ambao dini yao ni tawi la Waislamu wa mathehebu ya Shia lenye utambulisho na imani yake ya kipekee – wana shaka na serikali ya muda ya Rais Ahmed al-Sharaa licha ya ahadi zake za kuwalinda. Hadi sasa, mkoa wa Suweida ulikuwa umesalia chini ya udhibiti wa wanamgambo wa Druze ambao walikataa wito wa kujiunga na vikosi vya usalama.
Netanyahu amesema amejitolea kuzuia madhara kwa eneo la Druze nchini Syria kwasababu ya uhusiano wao wa kina na wale wanaoishi Israel na Milima ya Golan inayokaliwa na Israel.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.