Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA…..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

…na yule anayejenga Nyumba ya KAWAIDA.

Anayejenga ghorofa anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza kuinua ghorofa yake juu.

Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka unaweza kukuta yule anayejenga ghorofa bado yuko kwenye msingi.

Ila siku akianza kuinua ghorofa lake kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.

Kwenye maisha ndivyo ilivyo – “If want to go so high, you need to go so deep”

(Kama unataka kwenda juu sana ni lazima ukubali kwenda chini sana).

Ni lazima ufanye kitu cha tofauti kitakochokujengea future imara.

Ukweli ni kuwa watu wengi wanaokuzunguka wanajenga maisha ambayo ni kama nyumba ya kawaida.

Na wewe kama unataka kujenga maisha yanayofanana na ghorofa lazima ukubali kuonekana unachelewa kwenye baadhi ya mambo.

Hii inamaanisha utalazimika kufanya viti vya TOFAUTI na kuwa TAYARI kusubiri.

Utatakiwa kuwekeza wakati wengine wanaenda kununua nguo mpya waendane na fashion.

Utatakiwa kusoma vitabu wakati wengine wanaangalia movie na kupiga stories.

Utatakiwa uanzishe biashara yako wakati wenzako wamesharidhika na mshahara wanaopata n.k

Unachofanya kuanzia unapoamka hadi unapoenda kulala kitajulisha kama unajenga maisha GHOROFA ama ya KAWAIDA.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment