Wanyama huguswa na sauti za siri kutoka kwa mimea, wasema wanasayansi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wanyama huguswa na sauti zinazofanywa na mimea, utafiti mpya unapendekeza, na kufungua uwezekano kwamba mfumo wa ikolojia usioonekana unaweza kuwepo kati yao.

Katika ushahidi wa kwanza kama huo, timu katika Chuo Kikuu cha Tel Aviv iligundua kuwa nondo wa kike waliepuka kuweka mayai yao kwenye mimea ya nyanya kama ingetoa kelle walizohusisha na dhiki, ikionyesha kuwa wanaweza kuwa na afya mbaya.

Timu hiyo ya wanasayansi ilikuwa ya kwanza kuonyesha miaka miwili iliyopita kwamba mimea hupiga kelele ikiwa imefadhaika au inapokuwa katika hali mbaya.

Sauti hizo ziko nje ya masafa ya usikivu wa binadamu, lakini zinaweza kutambuliwa na wadudu wengi, popo na baadhi ya mamalia.

“Hili ni onyesho la kwanza la mnyama anayeitikia sauti zinazotolewa na mmea,” Prof Yossi Yovel wa Chuo Kikuu cha Tel Aviv alisema.

“Hizi ni tetesi tu katika hatua hii, lakini inaweza kuwa kwamba aina zote za wanyama watafanya maamuzi kulingana na sauti wanazosikia kutoka kwa mimea, wakati wa kuchavusha au kujificha ndani yake au kula mmea.”

Watafiti walifanya mfululizo wa majaribio yaliyodhibitiwa kwa uangalifu ili kuhakikisha kuwa nondo zinaitikia sauti na sio kuonekana kwa mimea.

Sasa watachunguza sauti ambazo mimea tofauti huzitoa na ikiwa spishi zingine hufanya maamuzi kulingana na sauti hizo, kama vile kuchavusha au kujificha ndani yake au kula mmea.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment