RSF yavamia soko la ng’ombe na gereza katika jiji la El-Fasher huko Sudan

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

RSF ilichapisha video kadhaa kutoka soko la mifugo kwenye mitandao ya kijamii
Maelezo ya picha,RSF ilichapisha video kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kudai kuwa imeteka soko la mifugo

Kundi la wanamgambo wa Sudan Rapid Support Forces (RSF) lilivamia mji uliozingirwa wa el-Fasher siku ya Ijumaa katika vita vilivyodumu kwa saa saba, walioshuhudia wameimbia BBC.

Wapiganaji wa RSF walifanikiwa kuteka soko la ng’ombe, gereza na kambi ya kijeshi huku wakionyesha video zao wakitembea kwenye mashamba yasio na watu.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wapiganaji wa RSF kuingia katika jiji la El-Fasher tangu lilipozingirwa- katika vita vinavyoendelea vya kuudhibiti mji huo wa magharibi wa Darfur miezi 15 iliyopita.

Siku ya Jumamosi asubuhi, jeshi lililipiza kisasi na kufanikiwa kuwarudisha nyuma wapiganaji wa RSF kupita mipaka ya el-Fasher.

Lakini Mathilde Vu, kutoka Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC), alielezea jiji hilo kama “mtego wa kifo”.

“Tunachosikia ni hadithi za kutisha za kigaidi na mashambulizi ya kila wiki, mashambulizi dhdidi ya miundombinu ya raia,” Bi Vu aliambia kipindi cha BBC.

“Kuna watu wa kujitolea wa ndani – wanajitahidi sana, wakihatarisha maisha yao kila siku kujaribu kutoa chakula kidogo kwa watu ambao wanakabiliwa na njaa.”

Mkazi wa el-Fasher Siddig Omar, mwenye umri wa miaka 65 aliiambia BBC kwamba wapiganaji wa RSF walivamia jiji hilo siku ya Ijumaa kutoka upande wa kusini na kusini-magharibi.

RSF, ambayo wapiganaji wake wamekuwa wakijificha kwenye mahandaki yaliyochimbwa kuzunguka mji huo, mara kwa mara hushambulia El-Fasher.

Kulingana na jeshi, hii ilikuwa shambulio lao la 220. Lakini safari hii, walifanikiwa kulidhibiti soko la mifugo la jiji hilo katika vita vilivyodumu kwa saa saba.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment