Kupungua kwa ufadhili kunahatarisha maisha ya mamilioni-UNAIDS

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) limesema kwamba kusitishwa ghafla kwa utoaji wa fedha kwa ajili ya kudhibiti virusi vya UKIMWI ni hali itakayosababisha “hatari” siku za usoni, ambayo inaweza kurejesha nyuma hatua ambazo zimepigwa kwa miongo mingi.

UNAIDS inakadiria kwamba huenda kukawa na maambukizi mapya ya virusi vya HIV milioni sita, na vifo milioni nne vinavyohusiana na UKIMWI kufikia mwaka 2029, kufuatia Marekani na wafadhili wengine kupunguza ufadhili wao katika harakati za kupambana na UKIMWI.

Shirika hilo lilitoa ripoti yake ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI tangu kuanza kupunguzwa kwa ufadhili huo.

Takwimu hizi kutoka UN zilikusanywa kabla ya Marekani kutangaza kupunguza ufadhili wake wa misaada mnamo mwezi Machi.

Lakini ni kielelezo cha athari kiasi gani zinaweza kutokea. Ulimwenguni kote, 40% ya watu walipata maambukizi ya VVU mwaka jana ikiwa ni kiwango cha chini kuliko miaka kumi na tano iliyopita; na kiwango cha vifo kinachohusiana na UKIMWI kimepungua na zaidi ya nusu.

Katika nchi za kusini mwa Afrika jangwa la Sahara, ambapo ugonjwa huo ulienea, ufadhili wa matibabu wa Marekani umesaidia kuongeza muda wa kuishi kwa miaka sita katika kipindi hicho hicho. Afrika Kusini ikiwa nchi inayopokea fedha nyingi zaidi kutoka Marekani.

Matokeo yake maambukizi mapya ya VVU yamepungua kwa asilimia 67 tangu kilele chake mwaka 2000.

Licha ya mafanikio makubwa katika kukabiliana na VVU mwaka 2024, kupungua kwa misaada kwa kiwango cha juu kwa ghafla hasa fedha za kukabiliana na VVU mwaka 2025, kumesababisha matatizo makubwa katika mifumo ya afya na kupunguzwa kwa wahudumu wa afya – kusitishwa kwa programu za kuzuia VVU, hatua ambayo inahatarisha huduma za matibabu za maambukizi ya UKIMWI.

Ufadhili mkubwa ukitoka kwa Shirika la Marekani la Misaada ya Kimataifa (USAID) ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake kwa tawala nne zilizopita kabla ya kusitishwa na Rais Trump.

‘’Ni ukatili, haijawahi kutokea kwa sababu, nchi zina changamoto tofauti hata matajiri, lakini huwezi kuondoa msaada unaookoa maisha kutoka kwa watu kirahisi tu. Unastahili kuweka mipango, na muda wa kipindi cha mpito,’’ Mkuu wa shirika la UNAIDS, Winnie Byanyima alisema.

UN inadai kupunguzwa kwa fedha hizo kunaweza kufanya jango hilo kuwa katika viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu miaka ya 2000.

Ili kuepuka hili, UN inasema nchi nyingi zaidi zitahitaji kuingilia kati na kusaidia kuweza kudumisha mafanikio ambayo yamepatikana kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment