Ukiwa CHINI Hautawaona…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Taji KICHWANI kwako na KITI cha MAMLAKA huwa vinavutia watu wengi sana.

Usisahau kuna watu ambao watakuwa na wewe UKUU wako unapokuwa UKO KAMILI.

Kuna maeneo mawili hautawaona:

Moja, hautawaona wakati wa MCHAKATO wa kutengenezwa kuwa mkuu.

Yaani unapopambana kukuza biashara…

Unapopigana vita ya kupanda juu HAUTAWAONA.

Ila ukishapata au kufika juu tu, basi utawaona.

Mbili, hautawaona siku UKIWA UMEPOTEZA ulichonacho.

Yaani, ukipoteza NAFASI, PESA au CHEO, wanahamia kwa mwingine.

Jifunze kwenye maisha kuwa, sio kila mtu atakuwa na wewe nyakati zote…

…hasa NYAKATI ZAKO NGUMU.

Hekima ni kujua kila mtu unamuweka wapi pale anaporudi, usijichanganye tena.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment