Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ugiriki imesitisha ushughulikiaji wa maombi ya kutafuta hifadhi kutoka Afrika Kaskazini kwa miezi mitatu baada ya kuongezeka kwa idadi ya wahamiaji.
Wanaowasili kwa boti kutoka eneo hilo watakamatwa na kuwekwa kizuizini, Waziri Mkuu wa kihafidhina Kyriakos Mitsotakis alisema.
Aliongeza kuwa Ugiriki ilikuwa “inatuma ujumbe uliodhamiriwa… kwa wafanyabiashara na wateja wao wote kwamba pesa wanazotumia zinaweza kupotea kabisa, kwa sababu itakuwa vigumu kufika Ugiriki kwa njia ya bahari.”
“Hali hii ya dharura inahitaji hatua za dharura vile vile kukabiliana nayo.”
Mitsotakis aliongeza kuwa masharti hayo yatatokana na hoja sawa za kisheria Ugiriki ilitumia mwaka 2020 kuwazuia maelfu ya watu kuvuka mpaka wa ardhi yao na Uturuki.
Rasimu ya sheria itawasilishwa bungeni siku ya Alhamisi.
“Ujumbe wa wazi: salia ulipo, kwa sababu hatutakukubali,” alisema waziri wa uhamiaji Thanos Plevris kwenye X.
Tangazo la Mitsotakis linafuatia ongezeko kubwa la wahamiaji wanaofika katika visiwa vya kusini vya Crete and Gavdos.
Zaidi ya wahamiaji 2,000 waliwasili Crete katika siku za hivi karibuni na wengine 520 waliokolewa nje ya pwani yake mapema Jumatano, na kufanya idadi ya jumla tangu kuanza kwa 2025 kufikia 9,000.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.