Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mji mkuu nchini Ukraine, Kyiv umeshambuliwa tena kwa ndege zisizo na rubani za Urusi usiku kucha, maafisa wa eneo hilo wanasema, takriban watu wawili wameripotiwa kuuawa na 13 kujeruhiwa huku moto ukiwaka katika mji huo.
Mamlaka ya Kyiv inasema mabaki ya ndege isiyo na rubani yalianguka kwenye paa la jengo la makazi katikati mwa wilaya ya Shevchenkivskyi.
Video kwenye mitandao ya kijamii, ambayo bado haijathibitishwa na BBC, inaonyesha milipuko angani usiku, huku vitengo vya ulinzi wa anga vikianza kukabiliana na shambulio hilo.
Jeshi la Ukraine pia limeonya kuhusu tishio la shambulizi la kombora la balestiki.
Ukraine iliripoti shambulio kubwa zaidi la anga kuwahi kutokea la Urusi Jumanne usiku, baada ya ndege zisizo na rubani 728 na makombora 13 ya balestiki kushambulia miji kote nchini humo mara kadhaa.
Jeshi la Urusi halijazungumza lolote kuhusu shambulio la hivi punde lililoripotiwa.
Huduma ya dharura ya Ukraine DSNS ilisema Jumatano jioni kwamba watu watatu waliuawa katika shambulio la anga la Urusi katika mji wa Kostiantynivka – karibu na eneo la vita mashariki mwa Ukraine.
Marekani ilianza tena kutuma baadhi ya silaha kwa Ukraine, Reuters iliripoti Jumatano jioni, siku chache baada ya kusitisha usafirishaji wa baadhi ya silaha muhimu.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alianzisha uvamizi wa Ukraine mnamo Februari 2022.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.