Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Marekani imetangaza mabadiliko makubwa katika sera yake ya viza za wasio wahamiaji wa Nigeria, ikipunguza muda na kuweka masharti ni mara ngapi Wanigeria wanaweza kuingia nchini humo.
Kuanzia Julai 8, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema kuwa karibu viza zote kwa wasio wahamiaji wala wanadiplomasia zinazotolewa kwa raia wa Nigeria sasa wataruhisiwa kuingia nchini humo mara moja tu, muda halali ukiwa miezi mitatu pekee.
Hatua hii ni sehemu ya marekebisho ya kimataifa ya ushirikiano, tofauti kabisa na masharti ya viza ya awali, ambayo mara kwa mara iliruhusu kuingia mara nyingi zaidi ya miaka miwili.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema sera za viza zitasalia “kuwa chini ya upitiaji upya unaoendelea” na zinaweza kubadilika kulingana na kukua kwa masuala ya kidiplomasia, usalama, na viwango vya uhamiaji.
Katika taarifa, serikali ya Marekani ilisema inafanya kazi kwa karibu na mamlaka ya Nigeria kuhakikisha nchi hiyo inakidhi viwango muhimu vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na:
- Kutoa hati salama za kusafiri
- Kusimamia suala la kupitisha muda wa viza, na
- Kushirikisha data za kiusalama au uhalifu kwa usalama wa umma.
Watalii wa Nigeria, wanafunzi na wasafiri wa kibiashara wanatarajiwa kuwa miongoni mwa wataoathirika zaidi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.