ICC yatoa vibali vya kukamatwa kwa viongozi wa Taliban kwa kuwatesa wanawake na wasichana

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) imetoa hati za kukamatwa kwa viongozi wawili wakuu wa kundi la Taliban, ikiwatuhumu kuwatesa wanawake na wasichana nchini Afghanistan.

Mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague ilisema kuna “sababu za kutosha” kuamini kuwa Kiongozi Mkuu Haibatullah Akhundzada na jaji mkuu Abdul Hakim Haqqani walifanya uhalifu dhidi ya binadamu kwa jinsi walivyowatendea wanawake na wasichana tangu kutwaa mamlaka mwaka 2021.

Katika kipindi chao, wameweka mfululizo wa vikwazo, ikiwa ni pamoja na wasichana zaidi ya 12 kutopata elimu, na kuwazuia wanawake kufanya kazi nyingi.

Ikijibu, Taliban ilisema haitambui ICC, ikiita hati hiyo “kitendo cha wazi cha uadui” na “matusi kwa wenye imani ya dini ya Kiislamu kote ulimwenguni”.

Pia kumekuwa na vikwazo juu ya umbali gani mwanamke anaweza kusafiri bila kuwa na mwanaume anayemsindikiza, na amri inayowakataza kupaza sauti zao hadharani.

Katika taarifa yake, ICC ilisema kwamba “wakati Taliban wameweka sheria fulani na marufuku kwa watu kwa ujumla, wamewalenga wasichana na wanawake kwa sababu ya jinsi zao, na kuwanyima haki na uhuru wa kimsingi”.

Umoja wa Mataifa hapo awali ulitaja vikwazo hivyo kuwa ni sawa na “ubaguzi wa kijinsia”.

Serikali ya Taliban imesema inaheshimu haki za wanawake kwa mujibu wa tafsiri yao ya utamaduni wa Afghanistan na sheria za Kiislamu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment