Kiongozi wa zamani wa Bangladesh aliidhinisha msako mkali, sauti iliyovuja yaonyesha

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Msako mkali dhidi ya maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi nchini Bangladesh mwaka jana uliidhinishwa na waziri mkuu wa wakati huo Sheikh Hasina, kulingana na sauti ya moja ya simu zake zilizothibitishwa na BBC Eye.

Katika sauti hiyo, ambayo ilivujishwa mtandaoni mnamo mwezi Machi, Hasina anasema aliidhinisha vikosi vyake vya usalama “kutumia silaha hatari” dhidi ya waandamanaji na kwamba “popote watakapowapata, watafyatua risasi”.

Waendesha mashtaka nchini Bangladesh wanapanga kutumia rekodi hiyo kama ushahidi muhimu dhidi ya Hasina, ambaye anashitakiwa bila kuwepo katika mahakama maalum ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Hadi watu 1,400 walikufa katika machafuko ya majira ya joto yaliyopita, kulingana na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa.

Hasina, ambaye alikimbilia India, na chama chake wanakanusha mashtaka yote dhidi yake.

Msemaji wa chama chake cha Awami League alikanusha sauti hiyo kuonyesha “nia yoyote iliyo kinyume cha sheria”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment