Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Ni lazima ufanye juhudi za kujua sababu ya msingi inayofanya uwe unapenda sana kughairisha mambo kwenye maisha yako.
ii. Ni lazima ukubali kuwa suala la kughairisha mambo kwenye maisha yako ni changamoto ambayo haswaa unataka kuitatua.
iii. Baada ya haya yote unatakiwa kupanga mpango unaoeleweka wa jinsi ambavyo unaweza kulitatua tatizo hili hatua kwa hatua.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo La Pili
– Ni lazima ukubali kuwa suala la kughairisha mambo kwenye maisha yako ni changamoto ambayo haswaa unataka kuitatua.
Hakuna namna unaweza kutatua tatizo ambalo haujakubali kwamba…
…unalo na hauko tayari kulitatua katika maisha yako.
Watu wengi sana huwa wanashindwa kutatua tatizo la kughairisha mambo kwa sababu…
…wamelifanya tatizo hili kuwa sehemu ya maisha yao na wamelikubali.
Hauwezi kutatua tatizo ambalo umelikubali liwe sehemu ya maisha yako.
Hivyo kabla haujafanikiwa kuishinda tabia ya kughairisha mambo kwenye maisha yako ni lazima…
…ujue kuwa ni tatizo na udhamirie kwamba unataka liondoke katika maisha yako.
Watu wengi sana huwa hawaweki mkazo wa kushughulikia tatizo la kughairisha mambo kwa sababu…
…hawajawahi kufikiria athari ambazo wanazipata kwa wao kughairisha mambo kwenye maisha yao.
Hebu fikiria ni mambo gani ambayo ungekuwa tayari umeyakamilisha…
…kama usingekuwa mtu ambaye unaghairisha mambo kila wakati?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.