Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais Donald Trump amechelewesha kutoza ushuru wa juu zaidi kwa bidhaa zinazoingia nchini Marekani, huku akituma barua kwa nchi 14 zikiwemo Japan na Korea Kusini kuelezea tozo mpya zinazowakabili.
Matukio ya hivi punde yanakuja wakati muda wa siku 90 ambao Ikulu ya White House iliweka kwa baadhi ya kodi zake kali zaidi za uagizaji bidhaa ulitarajiwa kuisha wiki hii.
Rais alirejelea tishio lake la kutoza ushuru wa 25% kwa bidhaa zinazoingia nchini kutoka Japan na Korea Kusini na kuandika barua zingine kwa viongozi wa ulimwengu kuonya juu ya ushuru kuanzia tarehe 1 Agosti.
Ushuru wa juu ulikuwa umepangwa kuanza kutekelezwa tarehe 9 Julai, baada ya kusitishwa hapo awali huku maafisa wa Ikulu wakisema wanalenga kuingia katika makubaliano ya kibiashara.
Alipoulizwa na mwandishi wa habari kama tarehe mpya ya Agosti ilikuwa tarehe ya mwisho, Trump alisema: “Ningesema ndio, lakini sio 100%.
Ikiwa watapiga simu na kusema tungependa kufanya kitu kwa njia tofauti, tutakuwa wazi kwa hilo.”
Pia siku ya Jumatatu, Trump alishiriki barua akiwahutubia viongozi wa nchi 14 kwenye mitandao ya kijamii, akiwafahamisha kuhusu mipango yake ya hivi punde ya ushuru, huku akiongeza kuwa viwango hivyo vinaweza kupanda au kushuka kulingana na uhusiano wetu na nchi yako”.
Viwango vingi vya ushuru vilivyoainishwa na Trump vilikuwa sawa na vilivyoainishwa mwezi wa Aprili, alipotoa tangazo lake la “Siku ya Ukombozi”, na kutishia wimbi la ushuru mpya kwa bidhaa kutoka nchi mbalimbali.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.