Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hamas inasema imetoa “jibu chanya” kwa wapatanishi juu ya pendekezo la hivi punde la usitishaji vita upya huko Gaza na kuwaachilia mateka makubaliano yaliyotolewa na Marekani.
Kundi la wapiganaji wa Palestina limeongeza katika taarifa yake kuwa “liko tayari kuingia mara moja katika duru ya mazungumzo”.
Afisa mkuu wa Palestina anayefahamu mazungumzo hayo aliiambia BBC kwamba Hamas ilikubali mpango huo lakini imeomba marekebisho kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na hakikisho la Marekani kwamba uhasama hautaanza tena ikiwa mazungumzo ya kumalizika kwa vita hivyo vilivyodumu kwa miezi 20 yatashindwa.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema siku ya Ijumaa kuwa kuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza ifikapo wiki ijayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.