Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji imeendelea usiku kucha huko Texas baada ya kutokea kwa mafuriko yaliyosababisha vifo vya takriban watu 24 na kuwaacha wasichana wengi wakiwa hawajulikani walipo kwenye eneo walilokuwa wamekita kambi ya Wakristo majira ya kiangazi.
Kulikuwa na onyo kidogo kwani Mto Guadalupe uliongezeka kwa futi 26 (7.9m) chini ya saa moja na mafuriko yakafuata yaliyosomba nyumba zinazohamishika, magari na maeneo yaliyokuwa yanatumiwa na watu kwa ajili ya likizo wikendi.
Vikosi vya uokoaji bado vinatafuta hadi watoto 25 ambao walikuwa miongoni mwa wasichana 750 waliokuwa wamekita kambi eneo hilo, nje kidogo ya mji wa Kerrville 104km (maili 64.0) kaskazini-magharibi mwa San Antonio.

Hali ya tahadhari imetamgazwa katika kaunti kadhaa ambapo barabara zimesombwa na maji na laini za mawasiliano zimekatika.
Rais wa Marekani Donald Trump aliutaja mkasa huo kuwa “wa kushtua” na “wa kutisha” huku Ikulu ikiahidi msaada wa ziada.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.