Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakuweza kupata mafanikio yoyote katika usitishaji mapigano nchini Ukraine wakati alipozungumza kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kambi ya jeshi la anga ya Andrews mjini Washington, Trump alisema alizungumzia vita vya Ukraine na Putin, pamoja na hali ya Iran.
“Hapana, sijapata mafanikio yoyote katika mazungumzo naye,” Trump alisema alipoulizwa kama alikuwa amekaribia zaidi makubaliano ya kusitisha mapigano.
Trump pia alisema “hahurahishwi ” na vita vinavyoendelea.
Mazungumzo kati ya Marais Vladimir Putin na Donald Trump yalichukua karibu saa moja, alisema msaidizi wa rais wa Urusi Ushakov.
Katika mazungumzo na Putin, Trump “alizungumzia tena suala la kukomesha haraka kwa hatua za kijeshi,” Ushakov alisema.
Kulingana na msaidizi wa Putin, mazungumzo ” yalikuwa ya wazi, kama biashara na thabiti.”
Mazungumzo ya mjini Istanbul yatasalia kuwa ya pande mbili kati ya Urusi na Ukraine, Ushakov aliongeza.
Kulingana naye, tarehe maalum za duru ya tatu ya mazungumzo mjini Istanbul hazikujadiliwa.
Putin alimwambia Trump kwamba Urusi haitalegeza msimamo wake wa kuondoa sababu za mzozo wa Ukraine, Ushakov alisema. Pia alisema kuwa mada ya kusimamisha usambazaji wa silaha za Marekani kwa Ukraine ilikuwa mojawapo.
Mbali na Ukraine, Putin na Trump walijadili hali inayozunguka Iran na Mashariki ya Kati kwa ujumla, kulingana na ripoti ya Ushakov.
Awali Rais wa Urusi alimpongeza Trump Siku ya Uhuru, ambayo huadhimishwa nchini Marekani mnamo Julai 4.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.