Kuna vita vingine usipigane…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ni ngumu sana KUSHINDA vita ya KUMPIGANIA mtu ambaye yeye mwenyewe AMEFANYA MAAMUZI ya KUONDOKA.

Kuna wakati lazima UPIME, aidha utumie nguvu zako kufanya bidii KUMBAKIZA au uzitumie KUANZA UPYA.

Usisahau kuna watu utaanza nao pamoja (Biashara, Urafiki, Mahusiano n.k), ila HAUTAMALIZA nao PAMOJA.

Usisahau kuwa, sik lazima wewe ndio uwe mwenye MATATIZO, wakati mwingine wao ndio wenye matatizo.

Usiingie kwenye MTEGO wa kujilazimisha KUMBAKIZA ambaye ameshaamua KUONDOKA.

Kwenye MAISHA kuna watu ambao tumepewa kwa ajili ya MAJIRA fulani, na yakishakamilika inabidi waende hata kama bado tunataka kuwa nao.

Jifunze kubaki na AMANI yako pale ambapo ulioadhania utabaki nao kwa muda mrefu wameamua kuondoka.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment