Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Israel imekubali masharti ya kusitisha mapigano Gaza kwa siku 60, Trump anasema
Israel imekubali “masharti ya lazima” ili kukamilisha usitishaji vita wa siku 60 huko Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump amesema.
Wakati wa makubaliano yaliyopendekezwa, “tutafanya kazi na pande zote kumaliza Vita”, Trump alisema katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, bila kuelezea masharti ni nini.
“Waqatar na Wamisri, ambao wamefanya kazi kwa bidii sana kusaidia kuleta Amani, watatoa pendekezo hili la mwisho. Natumai… kwamba Hamas itayakubali Makubaliano haya, kwasababu hayatakuwa mazuri – MAMBO YANAWEZA TU KUWA MABAYA ZAIDI,” Trump aliandika.
Israel ilianzisha kampeni ya kijeshi huko Gaza baada ya shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israel, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa. Takriban 56,647 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.
Haijabainika mara moja iwapo Hamas itakubali masharti ya kusitisha mapigano.
Tangazo la Trump linakuja kabla ya mkutano na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu uliopangwa kufanyika wiki ijayo, ambapo rais huyo wa Marekani amesema atakuwa “atakuwa na msimamo thabiti”.
Rais wa Marekani alisema Jumanne kwamba anaamini Netanyahu anataka kumaliza uhasama huko Gaza.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.