Waziri Mkuu wa Thailand asimamishwa kazi baada ya mazungumzo yake ya simu kuvujishwa.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Paetongtarn Shinawatra amesimamishwa kazi huku mahakama ya Thailand ikizingatia ombi la kutaka aondolewe.
Maelezo ya picha,Paetongtarn Shinawatra amesimamishwa kazi huku mahakama ya Thailand ikizingatia ombi la kutaka aondolewe.

Mahakama ya Katiba ya Thailand imemsimamisha kazi Waziri Mkuu Paetongtarn Shinawatra, ambaye anakabiliwa na shinikizo kubwa la kujiuzulu baada ya tukio la kuvujishwa kwa mazungumzo yake ya simu na kiongozi wa zamani wa Cambodia, Hun Sen.

Klipu hiyo, ambayo Paetongtarn alimwita “mjomba” na kumkosoa kamanda wa jeshi la Thailand, ilizua hasira miongoni mwa raia wa Thailand wengi wao wakiwasilisha ombi la kutaka afutwe kazi.

Mahakama sasa inazingatia hilo. Paetongtarn ni mwanasiasa wa tatu katika ukoo wenye nguvu wa Shinawatra – ambao umetawala siasa za Thailand kwa miongo miwili iliyopita – kupoteza mamlaka kabla ya kumaliza muda wao

Muungano wake unaotawala tayari una idadi ndogo ya wabunge baada ya mshirika mkuu wa kihafidhina kujiondoa wiki mbili zilizopita.

Mahakama ya Kikatiba ilipiga kura 7-2 kumsimamisha kazi wakati wakizingatia kesi ya kufutwa kwake na ana siku 15 za kuwasilisha utetezi wake.

Huku hayo yakijiri naibu Waziri Mkuu Suriya Jungrungruangkit atahudumu kama kaimu kiongozi wa nchi.

Ikiwa atafukuzwa kazi, Paetongtarn atakuwa waziri mkuu wa pili kutoka chama cha Pheu Thai kuondolewa madarakani tangu Agosti mwaka jana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment