Usipishane Na Majira Yako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye maisha kila mtu huwa ana majira yake ya KUVUKA kiwango.

Yaani, unaweza kufanya kitu kwa muda mrefu sana…

…ila kuna wakati ulioandaliwa na MUNGU wa kukuinua kwa KASI.

Mara nyingi majira haya yanapofika, kabla ya kuonekana kwa dalili za nje…

…huwa kunakuwa na dalili ya ndani ambayo ukiipuzia unaweza kuchelewa zaidi.

Kuna wakati utajisikia ndani yako KUCHUKUA HATUA fulani…

…au kufanya kitu ambacho sio cha kawaida.

Yaani, ni aina ya maamuzi ambayo wengine wakiyasikia wanashangaa na wanaweza wasikuelewe…

…Ila ndani yako unaona MSUKUMO WA JUU sana wa kufanya.

Ukifika katika hatua hii lazima UJIKAZE na uwe na UJASIRI.

Yaani, uamue kufanya hata kama MAZINGIRA ya nje hayasapoti.

Usisahau kuna vitu inabidi UANZE kuvifanya ili kusababisha mambo mengine yaanze KUTOKEA…

…ukichelewa utakuja kufanya MUDA sio rafiki.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment