Aina Tatu Ya Marafiki Wanaoua Ndoto Zako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Marafiki wanaoidharau / wanaoibeza ndoto yako

ii. Marafiki waharibu maono

iii. Marafiki wanaoshambulia ndoto yako

Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya kwanza ya Marafiki

– Marafiki Wanaoshambulia Ndoto Yako

Hawa ni watu ambao sio tu kwamba wanapuuzia na kuibeza ndoto yako…

…bali pia wanaishambulia ndoto yako.

Ni watu ambao wanakushambulia kwa maneno yao waziwazi kukuthibitishia kwamba hutaweza kuyafikia maono yako.

Mara nyingi watu hawa kwa sababu wanakujua wanaweza kuwapa taarifa zako watu wengine…

…ili wakushambulie na uonekane ni mtu ambaye huwezi ama hautafika mbali.

Ni muhimu sana kuelewa na kutambua kwamba aina hizi za marafiki zinapaswa kudhibitiwa mapema kabla ya kuleta madhara kwenye maisha yako.

Wakague marafiki ulionaoo, ujue kama una aina hizi za marafiki kisha uchukue hatua madhubuti.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment